Dakika 45 za kipindi cha pili, Yanga waliendelea kusaka goli la ushindi huku Ruvu shooting wakiwa wanatafuta la kusawazisha ambapo mpaka dakika 90 matokeo ni Yanga 2-0 Ruvu Shooting.
Timu ya Yanga imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu Tanzana Bara uliopigwa leo katika Uwanja wa Taifa.
Magoli ya Yanga yamefungwa na Simon Msuva kwa njia ya penati katika dakika ya 31 baada ya mchezaji wa Ruvu kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na Emanuel Martin akimalizia pasi safi ya Msuva kwenye dakika ya 90.
Katika dakika ya 45, Obrey Chirwa anapewa kadi ya nyekundu kwa makosa mawili baada ya mwamuzi kusema ameunawa mpira kabla ya kufunga na baadae kufanya utovu.
Baada ya matokeo haya Yanga wanaendelea kusalia katila nafasi ya pili wakiwa na alama 52 wakiwa nyuma ya Simba wenye alama 54.
Kipa wa Timu ya Ruvu Shooting, Bidii Hussein akiusindikiza kwa macho mpira uliowekwa wavuni na Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva katika mtanange wa Ligi kuu Tanzania bara, uliochezwa jioni ya leo uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 2-0.
Beki wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy akionyesha makeke yake mbele ya Beki mwinzie wa Timu ya Ruvu Shooting, Yusuph Nguya, katika mtanange wa Ligi kuu Tanzania bara, uliochezwa jioni ya leo uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 2-0.
Beki wa Timu ya Ruvu Shooting, Yusuph Nguya akimchezea rafu Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Simon Msuva, katika mtanange wa Ligi kuu Tanzania bara, uliochezwa jioni ya leo uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 2-0.
Kiungo wa kati wa Timu ya Ruvu Shooting, Shaibu Nayopa akimdhibiti vilivyo, Mshambuliaji wa Obrey Chirwa, katika mtanange wa Ligi kuu Tanzania bara, uliochezwa jioni ya leo uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 2-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...