Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji (R) Semistocles
Kaijage amewataka watumishi wa tume hiyo wazingatie maadili na kanuni za
utawala bora ili kutekeleza kwa ufanisi jukumu la Tume katika kukuza na
kuimarisha demkorasi na utawala bora nchini.
Jaji Kaijage ameyasema hayo alipoalikwa kuwa mgeni rasmi kufungua kikao
cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima jijini Dar es Salaam.
“Jukumu kubwa la Tume ni kukuza na kuimarisha demkorasi na utawala bora
nchini, kwa maana hiyo ni muhimu kwamba watumishi wa Tume wazingatie maadili na
kanuni za utawala bora ili kutekeleza kwa ufanisi jukumu hili” alisema na
kuongeza kuwa:
“Ni muhimu kwa watumishi wa Tume katika utendaji kazi wao kuepuka vitendo
vya ukiukwaji wa maadili kama vile rushwa, upendeleo na au ubaguzi wa aina
yoyote katika sehemu ya kazi”
Mbali na hayo, Mhe. Jaji Kaijage aliipongeza Tume kufanikisha uchaguzi
mdogo uliofanyika mwezi Januari mwaka huu katika jimbo la Dimani na kata 20 za
Tanzania Bara kwa kuufanya kuwa wa amani na utulivu pamoja na changamoto
mbalimbali zilizoukabili uchaguzi huo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima
Ramadhani (aliyesimama) akitoa neno la ukaribisho kwa Mgeni Rasmi wa ufunguzi
wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume hiyo Mhe. Jaji (R) Semistocles
Kaijage (kulia kwake) kabla ya kufungua kikao hicho.Kulia ni Katibu Mkuu wa (Tughe)
Taifa Bw. Heri Mkunda na kushoto ni Katibu wa Baraza hilo Bi. Rose Malo.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi.
Rose Malo akiwasilisha muhtasari wa kikao kilichopita cha baraza hilo huku
Mwenyekiti wa Baraza Bw. Kailima Ramadhani (katikati) na Naibu Katibu Msaidizi
Bi Uddy Sadiki wakifuatilia muhtasari wa kikao hicho.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...