Kampuni ya Ninayo kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Heifer International Tanzania ambalo limejikita katika kuondoa umasikini na matatizo ya njaa leo wameshirikiana katika kuwasaidia wakulima wa Tanzania kupata taarifa zote zinazohusu mauzo au manunuzi ya mazao mbalimbali kupitia mtandao wa Ninayo.com.

Ninayo ni jukwaa la mtandao wa kibiashara unaowawezesha wakulima kuuza, kununua au kuangalia bei elekezi za mazao mbalimbali yatokanayo na kilimo pia kuwapa uwanja mpana wa kulifikia soko la bidhaa hizo kwa urahisi.

Njia hii ya mtandao imejikita katika kutatua mambo makubwa matatu ikiwemo tatizo la kushindwa kwa mkulima katika usambazaji ambapo wanunuaji/wateja hawafahamu ni mazao ya aina gani wakulima wanauza, Mahitaji yasiyofahamika ambapo wakulima hawafahamu ni kiasi gani wanunuaji wapo tayari kununua mazao yao na kukosekana kwa utaratibu wa kuwaunganisha wanapohitaji kufanya biashara za mazao yao.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ninayo Jack Langworthy alisema matumizi ya intaneti yanazidi kukua kwa kasi sana nchini Tananzia, na hivi sasa intaneti imesambaa hadi vijiji maskini.

“Tunashukuru kwa kukua kwa kasi ya mitandao hasa kupitia simu za mkononi, ni uvumbuzi ambao umeleta mapinduzi katika kila sekta duniani, kuanzia kwenye bishara ya teksi, hoteli na zaidi sasa inaweza kupatikana kwa wakulima katika masoko ya Tanzania kukabiliana na mahitaji mahitaji mbalimbali ya chakula kwa bei elekezi kwa watu wote na hivyo kupunguza upotevu wa mazao mbalimbali”.
 
Afisa mtendaji mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya NINAYO Jack Langworthy akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya kuanzisha ushirikiano baina ya kampuni hiyo na shirika lisilo na kiserikali la Heifer utakaowawezesha wakulima kufikia masoko kupitia njia ya mtandao wa www.NINAYO.com .Kushoto ni Mkurugenzi mkazi wa Heifer International Tanzania Bi. Leticia Mpuya. 
Meneja uendeshaji wa kampuni ya NINAYO Bovan Mwakyambiki akiungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya kuanzisha ushirikiano baina ya kampuni hiyo na shirika lisolo na kiserikali la Heifer International Tanzania utakaowawezesha wakulima kufikia masoko kupitia njia ya mtandao www.NINAYO.com Kulia ni Afisa mtendaji mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya NINAYO Jack Langworthy.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...