Na Mboza
Lwandiko, Wshington DC
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Imeshiriki Mkutano wa mwaka wa 18 wa
Benki ya Dunia unaohusu masuala ya Ardhi na Umaskini, Machi 20 – 24, 2017 –
Washington DC – Marekani.
Mkutano
huo unaobeba ujumbe; “Utawala bora wa Ardhi”, umejumuisha zaidi ya wajumbe
1,200 kutoka nchi wanachama, zilizohusisha Serikali, taaluma, jamii na Sekta
binafsi mbalimbali.
Pamoja
na mambo mengine; Mkutano huo umejikita zaidi katika Maboresho mbalimbali
yanayoendelea kufanyika katika Sekta ya Ardhi Duniani, ikiwa ni pamoja na
kuzingatia nafasi ya takwimu na shuhuda zinazoashiria maboresho katika Sera za
Ardhi, na kuainisha Mikakati ya Maendeleo katika kuboresha zaidi Sekta ya
Ardhi.
Aidha,
Mada ambayo imewasilishwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
imewasilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara; Dkt. Yamungu Kayandabila, ambayo
ilibeba ujumbe - “Ardhi; Ufunguo wa
Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi kwa Tanzania”. Alieleza kuwa utawala wa
Ardhi Tanzania unazingatia; Sheria, Uwazi, Uwajibikaji na Ushirikishwaji wa
Wananchi. Pamoja na mengine Dkt. Kayandabila alieleza jitihada mbalimbali
ambazo zimekuwa zikifanyika kuboresha sekta ya ardhi nchini na juhudi ambazo
zinaendelea kuboresha utawala bora wa Ardhi nchini.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila
akiwasilisha mada: “Ardhi; Ufunguo wa Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi kwa
Tanzania”. Katika Mkutano wa 18 wa Benki ya Dunia wa masuala ya Ardhi na
Umaskini; Washington DC, Marekani.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila,
akiwa ameambatana na Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji;
Immaculate Senje, Kaimu Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya ;
Amina Rashidi, wakijadili jambo na wajumbe wenzao wa Mkutano wa 18 wa Benki ya
Dunia wa masuala ya Ardhi na Umaskini; Washington DC, Marekani
Wajumbe
kutoka Tanzania katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Finland kwenye mkutano
wa 18 wa Benki ya Dunia kuhusu masuala ya Ardhi na Umaskini uliofanyika mjini Washington DC, Marekani
Wajumbe
kutoka Tanzania wakifanya mazungumzo ya pamoja na mtaalamu mwelekezi wa Benki
ya Dunia kutoka nchini Uganda; Bwn. Moses Kibirige (aliyevaa miwani) kwenye
mkutano wa 18 wa Benki ya Dunia kuhusu masuala ya Ardhi na Umaskini uliofanyika
mjini Washington DC, Marekani
Katibu
Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila,
akiwa na wajumbe wengine kutoka nchi mbalimbali katika vikao vinavyoendelea
katika Mkutano wa 18 wa Benki ya Dunia kuhusu masuala ya Ardhi na Umaskini
uliofanyika mjini Washington DC,
Marekani. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...