Kampuni ya TDL maarufu konyagi imesitisha utengenezaji za pombe kwa kutumia vifungashio vya plastiki kwa mujibu wa agizo la serikali ambapo mwisho wa kusambaza pombe hizo ulikuwa jana.

Maofisa kutoka Mamlaka ya kusimamia vyakula na Madawa (TFDA),NEMC,TBS na Jeshi la Polisi wamefika kiwandani leo na kukuta hakuna uzalishaji wa vinywaji hivyo unaoendelea kama ambavyo kuna taarifa za kupotosha kwenye mitandao ya kijamii zinazoeleza kuwa TDL imekaidi agizo la serikali na imekutwa ikiendelea kufanya uzalishaji kwa kutumia vifungashio vilivyoipigwa marufuku na serikali.

TDL siku zote imekuwa ikiendesha shughuli zake za kibiashara kwa kufuata miongozo na sheria za serikali kupitia taasisi mbalimbali hiyo haiwezi kukaidi na kuendelea na uzalishaji wa kutumia vifungashio vya plastiki wakati vimepigwa marufuku bali inajipanga kutumia teknolojia za kutumia vifungashio vilivyotengenezwa kwa malighafi ya kioo ambavyo vina ubora  wa hali ya juu na salama kwa kuwa sio rahisi kuviigiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...