Wachimbaji wa mchanga unaodhaniwa kuwa na madini ya almasi ‘Wabeshi’ wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wameiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli iwatengee eneo maalum kwa ajili ya uchimbaji ili waache vitendo vya kuvamia mgodi wa almasi wa Williamson (Williamson Diamonds Ltd).


Wachimbaji hao wa madini ambao wamekuwa wakivamia mgodi na kuambulia kupigwa,kunyanyaswa na hata kuuawa na walinzi wa mgodi huo,walisema yapo maeneo ambayo hayatumiki hivyo ni vyema serikali ikawakatia maeneo ili iwe suluhu ya mgogoro kati yao na uongozi wa mgodi.

Wakizunguza na waandishi wa habari hivi karibuni kwa nyakati tofauti Wabeshi walisema wananchi wanaozunguka mgodi huo wamekuwa hawanufaiki nao kabla na baada ya uhuru hivyo wanaamini serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Magufuli itatatua kero yao ya muda mrefu.

Walisema vijana wengi wanategemea shughuli ya uchimbaji hivyo wakipewa eneo la uchimbaji wataweza kumudu gharama za maisha ikiwemo kutunza familia zao.

Mmoja wa wabeshi hao Mabula Njile mkazi wa kijiji cha Nyenze kata ya Mwadui Luhumbo alisema endapo serikali itawapatia maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo hawatavamia tena mgodi wa Williamson kwenda kuchimba mchanga unaodhaniwa kuwa na madini ya almasi.

Mkazi wa kijiji cha Nyenze kata ya Mwadui Lohumbo akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...