Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha 

WADAU na viongozi mbalimbali jimbo la Kibaha Vijijini,wamejitokeza kumuunga mkono mbunge wa jimbo hilo, Hamoud Jumaa kufanikisha ujenzi wa uzio wa kituo cha afya Mlandizi.

Ujenzi huo unatarajiwa kugharimu mil. 200 na ukikamilika utaondoa kero hiyo iliyodumu miaka mingi . Jumaa aliyasema hayo baada ya uzinduzi rasmi wa ujenzi huo ambapo hivi karibuni alianza kwa kuweka alama ya msingi.

Alieleza kwamba, wameshakubaliana na wananchi na wenyeviti wa vitongozi 26 kuwa kila kitongoji kitachangia sh.240,000 . “Madiwani kila mmoja atachangia 240,000 hivyo wanatarajia kukusanya zaidi ya sh. mil.4, mfuko wa jimbo sh. mil. 4 kununulia tofali zitakazoanzia ujenzi”alisema .

Hata hivyo,tayari wadau wamemkabidhi mifuko 500 ya saruji iliyogharimu sh. mil. 6, kokoto tani 7 kwa sh. mil. 9.1, mchanga mil. 2.4 tofali sh. mil 8.4, nondo tani moja sh. mil. 3.6.
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa akionyesha mifuko ya saruji 500 aliyochangiwa na wadau mbalimbali ili kusaidia katika ujenzi wa uzio wa kituo cha afya Mlandizi,ambao umezinduliwa rasmi 
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa akishiriki nguvu kazi na baadhi ya wananchi katika uzinduzi rasmi wa ujenzi wa uzio wa kituo cha afya Mlandizi .(picha na Mwamvua Mwinyi) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...