Wakulima wa alizeti Mkoani Singida wameazimia kuwa wazalishaji namba moja nchini wa alizeti kwa wingi na ubora wa hali ya juu kutokana na kutumia mbinu bora na za kisasa huku wakiachana na kilimo cha mazoea kilichowapa matokeo kidogo na yasiyo na ubora.

Wakulima wa Wilaya tatu za Iramba, Manyoni na Singida wamefikia uamuzi huo katika vikao kati yao na kamati ya ufuatiliaji wa progamu ya Uboreshaji wa Miundombinu ya Masoko, Uongezaji wa thamani ya mazao na Huduma za kifedha vijijini (MIVARF) iliyokuwa ikifanya tahmini ya mradi huo kwa kutembelea mashamba na kuzungumza na wakulima hao.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Mwangaza cha wakulima wa Alizeti kata ya Sanjaranda Wilayani Manyoni Bi. Janeth Emmanuel amesema, mradi wa MIVARF umewahamasisha kutumia mbegu ya alizeti ya kisasa aina ya record ambayo huzalisha wastani wa gunia 12 mpaka 16 kwa ekari moja wakati mbegu ya zamani ambayo walikuwa wakiitumia ya zebra imekuwa ikizalisha gunia mbili mpaka nne kwa ekari moja.

Bi Janeth amesema kutokana na wakulima wengi kuhamasika kutumia mbegu mpya ya record na kufuata elimu waliyopewa na MIVARF, Mkoa wa Singida utazalisha alizeti nyingi na bora kwa ajili ya viwanda vya ndani na nje ya Mkoa.


Afisa kilimo na Mratibu wa MIVARF Mkoa wa Singida akimsikiliza mkulima wa Alizeti Mkoa wa Singida akipalilia zao hilo, mkulima huyu amefuata ushauri wa kitaalamu wa kupanda kwa mistari, kuweka mbolea na kutumia mbegu mpya ya record ambayo huzalisha kwa wingi.
Mkulima wa Alizeti Mkoa wa Singida akipalilia zao hilo, mkulima huyu amefuata ushauri wa kitaalamu wa kupanda kwa mistari, kuweka mbolea na kutumia mbegu mpya ya record ambayo huzalisha kwa wingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...