Frank Mvungi-Maelezo

Watanzania wametakiwa kujitolea kuchangaia Damu ili kuwasaidia wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa moyo wanaohitaji kuongezewa damu wakati wa kupatiwa mat

ibabu.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo na Daktari Bingwa wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

“Tunatarajia kuwa na kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 3/4/2017 hadi tarehe 7/4/2017 ambapo Taasisi yetu itashirikiana na Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Healinga Little ya London Uingereza.”Alisisitiza Dkt. Nyangasa

Akifafanua Nyangasa amesema kuwa wagonjwa 12 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kipindi hicho kwa ushirikiano na Madaktari hao kutoka Taasisi ya Healing Little ya London Uingereza.

Kufuatia upasuaji huo Dkt. Nyangasa amewaomba wananchi kuendelea kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya wale wanaohitaji kuongezewa damu.

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imekuwa Moja ya Taasisi Bora katika ukanda wa Afrika mashariki na Kati katika kutoa matibabu moyo kwa wagonjwa kutoka hapa nchini na katika mataifa mbalimbali yanayoizunguka Tanzania.

Upatikanaji wa damu yakutosha imekuwa moja ya changamoto zinazoikabili Sekta ya afya kutokana na mwitikio mdogo wa wananchi kujitolea damu ili kusaidia wale wenye uhitaji hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kuunga mkono juhudi za Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika kuhamasisha wananchi kujitolea kuchangia damu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...