Akizungumza katika katika ziara yake mkoani Tanga iliyoingia siku ya tano Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba amesema kuwa ni vema rasilimali za nchi hii zitunzwe kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.”hatuwezi kufanikiwa kama tutaharibu mazingira” Makamba alisisitiza.

Waziri Makamba amesema ofisi yake ya imedhamiria kuchukua swala la mazingira kwa uzito wa kipee ikiwa ni pamoja na kuweka hifadhi ya mazingira katika mipango ya maendeleo.” Uwekezaji wote lazima uende sambamba na hifadhi ya mazingira”

Aidha, uongozi wa Halmashauri ya Mji Korogwe imetakiwa kuwachukua hatua kali wananchi wote wanaofanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji, kwa kutumia sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na ile ya maji ya mwaka 2009. Waziri Makamba amesema kuwa ofisi yake iko katika hatua za mwisho za kuteua wakaguzi wa mazingira 200 ambao watapata mafunzo na kusambazwa katika Halmashauri mbali mbali nchini.

Pia Waziri Makamba amesema kuwa katika kikao kijacho cha Bunge Ofisi ya Makamu wa Rais itatoa waraka juu ya usimamizi na uchimbaji wa mchanga nchini pamoja na umiliki wa “Chain-saw” kwa lengo kuweka utaratibu utakaowezesha kutambua na kutoa vibali maalumu kwa shughuli hizo ili kulinda mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba ameendelea na ziara yake maalumu ya kukagua shughuli mbalimbali za kimazingira nchini na hii leo amepokea taarifa ya hali ya mazingira katika Halmashauri ya Mji Korogwe na Same.

Awali akimkaribisha Waziri Makamba, Mwenyekiti wa Halmashauri ya hiyo Bw. Hillary Ngonyani amesema kuwa katika kutekeleza sheria ya mazingira zoezi la uzoaji na utupaji wa taka ngumu na taka maji umewekewa mkakati maalumu na kutekelezwa kikamilifu pia usafi wa mazingira umefanyika kwa kufanya ukaguzi wa nyumba hadi nyumba na kutoza faini kwa wananchi wasio na vyoo.

Bw. Ngonyani amebainisha kuwa wananchi wanaokiuka taratibu hizo hushtakiwa kwenye mabaraza ya kata na kupewa muda maalumu wa kujenga vyoo, kusisitizwa kuvitumia pia kuamriwa kusafisha mazingira yao chini ya uangalizi wa maafisa afya.

Aidha Bw. Ngonyani amesema kuwa wananchi wamekumbusha pia kutofanya shughuli za maendeleo kando ya mito na vyanzo vya maji ili kupunguza athari kwa mazingira, na kuunda kwa kamati za mazingira.

Katika hatua nyingine Bw. Ngonyani ameinisha changamoto zinazojitokeza katika Halmashauri ya Korogwe mji kuwa ni pamoja na Ukosefu wa wakaguzi wa Mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha vipindi vya mvua kubadilika na kuongezeka kwa joto.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiandaa mti kwa ajili ya kuupanda ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kampeni ya upandaji miti nchini. Zoezi hilo limefanyika leo katika Halmashauri ya mji Korogwe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na wawakilishi wa wananchi, watumishi na Watendaji wa Halmashauri ya Mji Korogwe (hawapo pichani). Waziri Makamba amesisitiza umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na hifadhi ya mazingira kwa ujumla wake.
Sehemu ya wawakilishi wa wananchi, watumishi na Watendaji wa Halmashauri ya Mji Korogwe wakimsikiliza Waziri Makamba alipofanya ziara ya kikazi kutembelea Halmashauri hiyo, kusikiliza na kujionea changamoto za kimazingira na kuainisha namna bora ya kukabiliana nazo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...