Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  akitoa Maelekezo kwa  Watendaji Wakuu wa  Wizara yake wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni sehemu ya maandalizi  muhimu  kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kushoto ni  Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. 
 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  akiwa pamoja na Watendaji Wakuu wa  Wizara yake wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo.  
 Baadhi ya Watendaji Wakuu wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakipitia bajeti za taasisi zao,  ikiwa ni sehemu ya maandalizi  muhimu  kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa [NIDA] Massawe, akifuatiwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr.  Anna Peter Makakala, watatu kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye na wanne ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Dr. Juma Malewa. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.   
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...