Na Lulu Mussa,Mwanga - Kilimanjaro
Imebainika kuwa Ziwa Jipe liko hatarini kutoweka endapo hatua za haraka hazitachukuliwa katika kulinusuru. Hayo yamesemwa na Waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa Mazingira Mh. January Makamba alipofanya ziara ya kukagua ziwa hilo ambalo sehemu kubwa imezungukwa na magugu maji.
Waziri Makamba amesema kuwa ziwa hilo ni rasilimali muhimu na hivyo ni lazima kuwe na mpango wa muda mfupi na ule wa muda mrefu. Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamiza wa Mazingira (NEMC) ameazimia kutangaza kupita Tangazo la Serikali kuwa eneo hilo ni eneo nyeti kimazingira."Tutatanga eneo hili kuwa eneo nyeti kimazingira na tutaweka masharti ya matumizi katika eneo hili" Alisisitiza Makamba.
Azimio hilo la kutangaza kuwa eneo mahsusi ama nyeti kimazingira itasaidi katika kuandika maandiko mbalimbali ya miradi na kupata fedha kutoka kwa wadau na washirika wa maendeleo. Pia litawekwa chini ya uangalizi maalumu na kuweka masharti ya matumizi bora ya eneo hilo. " Tutaweka masharti makali na magumu zaidi ili watakao kiuka wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria" Aliongezea Waziri Makamba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Mtendaji wa Kijiji cha Butu,
Kata ya Jipe Wilayani Mwanga Bw. Nassor Abdul wakati Waziri Makamba
alipotembelea Ziwa Jipe ambalo limeathiriwa kwa kiasi kikubwa na magugu maji
ambayo yanasababisha kupungua kwa shughuli za uvuvi ambazo ndio chanzo kikubwa
cha mapato kwa wakazi wa eneo hilo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw.
Aron Mbogho.
Mifano kwa vitendo: Pichani Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwa amembeba
mtoto Meshack Ombeni katika Kijiji cha
Butu pembezoni mwa Ziwa Jipe. Waziri Makamba amewaasa wananchi hao kulinda Ziwa
hilo ili liweze kunifaisha vizazi vijavyo na kuwatahadharisha kuwa uharibifu wa
mazingira utahatarisha uhai wa ziwa hilo. .
Upungufu mkubwa maji katika bwawa la nyumba ya
Mungu. Inasemekana kupungua kwa kina cha maji kunatokana na ukame wa muda mrefu
na uharibifu mkubwa wa mazingira
kutokana na shughuli za binadamu katika vyanzo vya maji vinavyopeleka maji
katika bwawa hilo ukiwemo Mto Kikuletwa.
Kwa tarifa kamili BOFYA HAPA
Kwa tarifa kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...