Kamati
za maji za visima kumi vya maji katika manispaa ya Singida zimekuwa
sababu ya miradi hiyo iliyokamilika kwa asilimia miamoja kutofanya kazi
na kuwanufausha wananchi huku ikiwa imegharimu fedha nyingi za serikali
na wahisani hasa benki ya dunia.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa
Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mwishoni mwa wiki hii mara baada ya
kukagua miradi hiyo na kujiridhisha kuwa miradi hiyo imekamilika licha
ya kutofanya kazi.
Dkt. Nchimbi amesema sababu kubwa ya kutofanya
kazi miradi hiyo ni udhaifu wa kamati za maji na wanasiasa katika
maeneo ya miradi kutojali shida ya wananchi ya kukosa maji na hivyo
kuitelekeza miradi hiyo badala ya kuisimamia.
Amesema lengo la
miradi hiyo ni wananchi wapate maji safi na salama kwa umbali usiozidi
kilometa nne kama ilivyoagizwa na serikali.
“Katika ukaguzi wangu
nimebaini mifumo katika miradi hii ya maji ipo vizuri sana. Baadhi
inaendeshwa kwa umeme na mingine kwa mafuta ya dizel. Makubaliano
yalikuwa baada ya kukamilika miradi hii iendeshwe na kamati za maji kwa
asilimia mia moja”, amesema.
Dkt. Nchimbi amesema wajibu wa
kamati hizo ni pamoja na kukusanya fedha zinazotokana na kuuza maji kwa
wateja pamoja na matengenezo ya miundombinu ya visima hivyo ili miradi
hiyo iwe endelevu.
“Fedha zinazopatikana ndizo zitakazoendesha
mradi husika ikiwemo kugharamia matengenezo ya mashine, pampu,
miundombinu, kununulia dizel, umeme na kumlipa mhudumu wa mradi.
Makubaliano ni miradi ikikamilika inabaki mikononi mwa wananchi kupitia
kamati zao za maji. Serikali na wafadhili hawatahusika tena”,
amesisitiza Dkt. Nchimbi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...