Jovina Bujulu- MAELEZO. 

Ukuaji wa uchumi katika nchi nyoyote duniani hujengwa na sekta mbalimbali ikiwemo madini, utalii, misitu na makusanyo ili kuwahudumia wananchi katika mahitaji yao ya kila siku.

Miongoni mwa huduma ambazo hutolewa baada ya makusanyo ya mapato yatokanayo na sekta hizi yanasaidia kuboresha utoaji wa elimu, afya, maji na nishati kwa manufaa ya wananchi.

Sekta ya madini nchini imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi na shughuli mbalimbali za maendeleo kupitia uwekezaji, ikiwemo ujenzi wa miundombinu muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, hivyo kuwa na mchango chanya katika kuinua kipato cha nchi na wananchi kwa ujumla.

Ili sekta madini iwe na tija kwa nchi na wananchi wake, Serikali imeweka mamlaka ya kuratibu ili kuhakikisha kuwa makampuni ya uchimbaji madini yanafanya shughuli zake kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Mchango wa makampuni haya umekuwa na tija kwa taifa kwa kutengeneza ajira pamoja na kulipa kodi zinazostahili kulipwa, kuchangia soko la fedha za kigeni, manunuzi ya huduma pamoja na michango ya hiyari kwa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa jamii zinazozunguka makampuni hayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania ya mwaka 2015, inaonyesha kuwa sekta rasmi ya uchimbaji madini ilitoa ajira 7,355 ambazo ni za moja kwa moja na zaidi ya ajira 3,000 kupitia makampuni ya wakandarasi.

Upatikanaji wa ajira hizo unaonesha kuwa mtu mmoja aliyepata ajira anahudumia watu 11 wasio na kazi na hivyo kuwezesha wastani wa watu 114,000 kuendelea kuishi na kupata huduma za msingi.

Kwa upande wa kulipa kodi, taarifa hiyo inaonyesha kuwa kati ya mwaka 2009 na 2015 makampuni makubwa yamelipa kodi Serikalini zaidi ya shilingi billioni 870 ikiwa ni mrahaba na zaidi ya shilingi billioni 680 zililipwa kama kodi ya mapato na kodi nyinginezo ambazo sio za moja kwa moja.

Aidha, katika kipindi cha mwaka 2015 pekee, shilingi billioni 146 zililipwa na migodi mikubwa mitano ya dhahabu pamoja na mgodi mmoja wa almasi kama mrabaha na kodi ya mapato.

Uendeshaji wa sekta ya madini nchini upo chini ya Serikali na taasisi zake ambazo ni Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Shirika la Uchimbaji wa Madini la Taifa (STAMICO), ambapo sera zilizowekwa mwishoni mwa miaka ya 1990 ziliwavutia wawekezaji wageni ambao walianzisha migodi mikubwa ya uchimbaji wa dhahabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...