Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

TAASISI ya Tulia Trust inayomilikiwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson imewafadhili wanafunzi 27 kwa ajili ya kupata mafunzo ya sanaa.

Taasisi hiyo imewadhamini wanafunzi hao kutoka Mbeya kusoma kwenye chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa), kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani.

Wanafunzi hao watapata fursa ya kujifunza sanaa ya maonyesho ya upigaji ngoma za asili, maigizo na utumiaji jukwaa.Akizungumza kwenye uzinduzi wa kuwakabidhi wanafunzi hao chuoni hapo, Dkt. Tulia amesema lengo la kuwafadhili vijana hao ni kutokomeza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana.

Amesema taasisi yake imedhamilia kukuza sanaa kwa vijana nchini ili kutatua tatizo la ajira na kuongeza ufanisi kwenye vipaji vyao walivyokuwa navyo awali.Alisema vijana hao wakipata mafunzo kwenye chuo hicho wataweza kufanya shughuli zao za ngoma za asili kiutaalamu zaidi, hali itakayowaongezea kipato na kuwafungulia fursa nyingi.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya Vikundi vya  ngoma za asili kutoka mkoa mbeya yanayofadhiliwa na Tulia Trust.

Mtendaji mkuu wa chuo cha Sanaa Bagamoyo(TASUBA) akizungumza kumkaribisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, akicheza ngoma pamoja na Mtendaji mkuu wa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo , Dk Herbert Makoye.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson akiwasili katika chuo cha Sanaa Bagamoyo kwa jili ya ufunguzi wa mafunzo kwa vikundi vya Sanaa mkoa mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...