SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limetoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa kituo cha Afya katika Kata ya Muhukuru, Kijiji cha Matama, Mkoani Ruvuma.

Vifaa hivyo, ni mifuko 800 ya saruji na nondo 400 zitakazosaidia kufanikiwa ujenzi wa kama njia yakuleta maendeleo katika jamii.Katika kufanikisha ujenzi huo, NSSF imetoa mifuko 800 ya saruji pamoja na nondo zipatazo 400.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji, alisema NSSF ni shirika kubwa la hifadhi ya jamii lenye ofisi katika kila mkoa wa Tanzania na wilaya zake.

Mpango wa ujenzi wa zahanati hiyo umetokana na ombi la Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa NSSF kuona jinsi ya kusaidia jamii inayoshi katika Kata ya Muhukuru ambao walikuwa wanatumia kilometa 62 kufika katika zahanati ya Muhukuru.

Msaada huo wa NSSF, unalenga kufanikisha mpango huo wa kuwapa wananchi unafuu wa kupata huduma za afya, hivyo kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya kukabidhi vifaa vya ujenzi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini, Oraleti Komando aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Naye Diwani wa Kata ya Muhukuru, Manfred Mzuyu alisema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka kwani baada ya kukamilika, utapunguza kero wanayopata wakazi wa kijiji cha Matama.

Aidha, diwani huyo aliongeza kuwa ujenzi huo utasimamiwa kwa ukaribu kuhakikisha hakuna atakayehujumu ujenzi wa kituo hicho na kutoa wito kwa wengine kuiga mfano huo wa NSSF.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Oraleti Komando, akipokea sehemu ya msaada wa mifuko 800 ya saruji na nondo 400 kutoka kwa Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji. Hafla hiyo ilifanyika mkoani Ruvuma mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini, Oraleti Komando, akimkabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na NSSF kwa Diwani wa Kata ya Muhukuru, Manfred Mzuyu. Kulia ni Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji.

Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji (wa tatu kulia), Ofisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano, Amina Mmbaga (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wengini wa NSSF baada ya kukabidhi mifuko 800 ya saruji pamoja na nondo 400 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Matama, Songea.
Wakzi wa Kijiji cha Matama Kata ya Mahukuru wakiwa katika hafla hiyo.
Sehemu ya msaada wa mifuko ya saruji iliyotolewa na NSSF kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Matama, Songea mkoani Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...