Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Mhandisi Raymond Mbilinyi akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam juu ya uzinduzi wa Baraza la Taifa la Biashara ambapo litakuwa ni Baraza la tatu katika kipindi cha awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye.

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuzindua Baraza la Tatu la Taifa la Biashara (TNBC), Mei 6 mwaka huu ambapo pia kutafuatiwa na Mkutano wa kumi wa Baraza hilo.

Baada ya uapisho, Desemba 2015 Rais Magufuli alianza kukutana na kundi la Wafanyabiashara nchini, hata hivyo Mwezi August, 2016 Rais Magufuli aliteua Wajumbe 20 kutoka Serikalini na 20 kutoka Sekta Binafsi kuunda Baraza hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Mhandisi Raymond Mbilinyi amesema mada zitakazo kuwepo katika mkutano huo ni zingatia ukuaji wa Kilimo, ukuaji wa Viwanda na ushiriki wa sekta binafsi katika ujenzi wa viwanda, pia namna ya kuboresha majadiliano kati ya sekta binafsi na sekta ya Umma ili kuwa karibu.

Amesema juhudi nyingi zinafanyika na Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara, ikiwa pamoja na kuunda Kamati iliyokuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu inayoangalia maboresho ya mazingira ya biashara nchini. Pia kuwepo na Kamati nyingine muhimu iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji inayoangalia maboresho ya kisera.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye ametoa wito kwa Mawaziri kufanya majadiliano na Sekta binafsi katika sekta zao ili kuangalia changamoto zipi zinakwamisha uwekezaji ambao utatupeleka katika uchumi wa Viwanda ifikapo 2025. Pia amewataka Wakuu wa Mikoa kufanya mabaraza ya biashara, mikutano ya mabaraza ya biashara kuleta hali ya mazingira ya uwekezaji nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akitoa ufafanuzi kuhusiana na Mawaziri kufanya majadiliano na Sekta binafsi katika sekta zao ili kuangalia changamoto zipi zinakwamisha uwekezaji.
Sehemu ya Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano huo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...