Wazazi
wanaoshindwa kuwapeleka watoto kupata huduma za chanjo wanakiuka haki
za binadamu hasa haki ya kuishi na pia wanaenda kinyume na juhudi za
serikali za kupambana na maradhi, umaskini na ujinga.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesea hayo katika hotuba yake
iliyosomwa na Mwakilishi wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo
wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo uliofanyika mapema leo katika
hospitali ya Sokoine Manispaa ya Singida.
Dkt.
Nchimbi amesema watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano
wanapaswa kupata chanjo zote ili kuwakinga na magonjwa ya homa ya ini,
surua, nimonia, kuhara, kifua kikuu, na pepopunda ambayo yanazuilika kwa
chanjo na motto akiugua kupona ni nadra
“Mtoto
akiumwa magonjwa hayo kwa kukosa chanjo kupona ni majaliwa na akipona
anaweza kupata ulemavu wa kudumu, hivyo nawasisitiza msipuuze mzingatie
kukamilisha chanjo zote” amesisita
Ameongeza
kuwa serikali imekamilisha wajibu wake kwa kuhakikisha chanjo zote
zinapatikana na hivyo umebaki wajibu wa kila mzazi na mlezi kuhakikisha
motto anapata chanjo pamoja na kuwaelimisha na kuwafichua wale
wasiowapeleka watoto kupata chanjo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akitoa chanjo kwa mtoto wa umri wa siku nne ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida mapema leo katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akifurahi mara baada ya kutoa chanjo kwa mtoto wa umri wa siku nne ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida mapema leo katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao waliojitokeza katika hospitali ya Sokoine Manispaa ya Singida wakishiriki uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...