Bwana harusi John Focus Lyimo akimlisha ndafu mkewe   Bernadetha Francis Munishi   kwenye mnuso wa nguvu walioandaa kusherehekea harusi yao katika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jijini Dar es Salaam Jumamosi. Harusi yao ilifungwa katika Kanisa Katoliki la Mt. Rita wa Kashia, Kimara Temboni kabla ya hafla hiyo.
Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi (kulia) akimlisha keki mumewe John Focus Lyimo kwenye hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Harusi yao ilifungwa katika Kanisa Katoliki la Mt. Rita wa Kashia, Kimara Temboni. Bwana harusi, John Focus Lyimo (katikati) akiandaa ndafu maalum kwa ajili ya kumlisha mkewe ikiwa ni ishara ya kumkaribisha nyumbani mara baada ya ndoa yao. Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi pamoja na wapambe wao wakiwa kwenye hafla hiyo.Bwana harusi, John Focus Lyimo (wa pili kushoto) akimtambulisha mkewe Bi. Bernadetha Munishi (wa pili kulia) kwa wageni waalikwa kwenye hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Waliokaa ni wapambe wa maharusi.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...