Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya imesema itawashughulikia wakurugenzi wote wa halmashauri ambao wataonekana kuwa chanzo cha ukosefu wa huduma bora za mama na mtoto katika hospitali za Wilaya na vituo vya afya kote nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu alipokuwa akifungua mkutano wa 24 wa Madaktari bingwa wa magonjwa ya Wanawake na Watoto (AGOTA) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

“ swala la afya ya mama na mtoto ni lililopewa kipaumbele kwa serikali ya Tanzania na Dunia kwa ujumla hivyo wakurugenzi wa halmashauri wanao wajibu wa kuhakikisha wanaboresha huduma hizi kwani ni vitu vidogo ambavyo vipo ndani ya bajeti yao, tutawachukulia hatua wakurugenzi wote ambao watashindwa kutimiza wajibu wao katika kulinda afya ya mama na mtoto” amesema Waziri Ummy.

Amesema zipo changamoto nyingi katika huduma hizi hivyo katika bajeti ya 2017/2018 wizara yake imetenga fedha za kutosha kwa ajili ya huduma za uzazi wa mpango ili ziwe bora na kuepuka kero ya wanawake wanaopata huduma hii kupanga foleni.

Ametaja kuwa katika tafiti inaonyesha kuwa ni wanawake 32 tu kati ya 100 ndio ambao wanatumia huduma ya uzazi wa mpango hivyo serikali itatumia njia nzuri zaidi kuwafikia wanawake wengi.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Madaktari bingwa wa masuala ya afya ya Mama na Mtoto (AGOTA), Prof Andrea Pembe amesema kuwa serikali imefanya kazi kubwa sana katika utoaji wa huduma katika vituo vya afya Tanzania .

Ameongeza kuwa uelewa mdogo wa jamii juu ya masuala ya afya ya uzazi yamechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa vifo vya Mama na mtoto.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Watoto na wanawake nchini AGOTA wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 24 wa Taasisi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar leo.
Rais wa Shirikisho la Madaktari bingwa wa masuala ya afya ya Mama na Mtoto (AGOTA), Prof Andrea Pembe, akizungumza kabla ya kumkaribisha waziri Ummy Mwalimu kwa ajili ya ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar leo.
 Daktari Gileard Masenga kutoka Hospitali ya KCMC Moshi akitoa taarifa fupi juu ya tafiti iliyofanywa kuhusiana na Afya ya Mama na Mtoto nchini kwenye mkutano wa 24 wa Madaktari bingwa wa magonjwa ya Wanawake na Watoto (AGOTA) uliofanyika leo.
 Baadhi ya Madaktari walioshiriki mkutano wa 24 wa Madaktari bingwa wa magonjwa ya Wanawake na Watoto (AGOTA) wakifutilia mada zilizokuwa zinatolewa leo.
Waziri Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...