Na. Immaculate Makilika- MAELEZO - DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Ajira na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama amewaasa Watanzania kuwa wazalendo pamoja na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.

Akizungumza, leo mjini Dodoma wakati akifuatatilia maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika Aprili 26 mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma.

“Tunapoadhimisha miaka 53 ya Muungano ninawaomba watanzania kuwa wazalendo pamoja na kulinda amani ya nchi” alisema Waziri Mhagama

Pia, Waziri Mhagama aliwaomba watanzania hasa wakazi wa Dodoma kuhudhuria kwa wingi katika Maadhimisho hayo yatakayofanyika jumatano wiki hii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema kuwa mkoa wake umejipanga vizuri katika kufanikisha maadhimisho hayo, ambapo pia alivishukuru vyombo vya habari kwa kuhamasisha wananchi juu ya maadhimisho hayo.

“Wananchi wamehamasika kushiriki katika maadhimisho haya ya miaka 53 ya Muungano, ninawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya na tunaamini mtaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika maadhimisho hayo” alisema Rugimbana

Maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yamehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, ambapo pia yatahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali.

Maadhimisho hayo ya miaka 53 ya Muungano yanatarajiwa kupambwa namaonesho kutoka kutoka vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama, burudani za vikundi vya ngoma pamoja na maonesho ya halaiki.

 Waziri Mhagama akikagua maandalizi ya kuadhimisha Sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika viwanja vya Jamhuri  leo Mjini Dodoma.
 Baadhi ya wananchi wakifuatilia maonesho ya maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma kwa mara ya kwanza tangu Serikali ilipohamia Dodoma.
 Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.

 Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.

 Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...