Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii. 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kushiriki tukio la uvamizi wa Mkutano wa wanachama wa CUF uliofanyika Vinna Hotel Mabibo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa Habari jijini hapa. Amesema kuwa. Aprili 22 mwaka huu majira ya mchana, walipokea taarifa ya kuwa watu wasiofahamika wakiwa na silaha walivamia mkutano huo na kujeruhi baadhi ya watu. 

Kamanda Sirro ameongeza kuwa, mpaka sasa watuhumiwa watatu waliokamatwa wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika hatua za kisheria zitafuatwa juu yao na amewasihi watu kutii sheria bila shuruti kwani hakuna mtu au kikundi chochote cha watu wanaoweza kuwa na mamlaka ya kushambulia wengine. 

"Kama unamalalamiko pitia polisi, au mahakamani siyo kuvamia kundi la watu wengine kama wako juu ya sheria, tunafuatilia wale wote waliohusika katika kufanya shambulio hilo na mtu mmoja aliyejeruhiwa sana anataja watu walioshambulia" amesema Sirro. 

Kamanda Sirro, amesema jeshi la polisi linaamini kuwa watu waliofanya uvamizi huo walifanya kwa utashi wao wenyewe na kwamba pindi upelelezi ukikamilika watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani. 

Aidha amewaonya baadhi ya viongozi wa CUF waliotangaza kuwafuata watu fulani na kuwawajibisha ni vema wakumbuke kuwa hakuna mtu aliyeko juu ya sheria kwani hakuna mtu aliyeko juu ya mamlaka. 

Mapema wiki iliyopita, watu wasiojulikana wakiwa na bastola walivamia mkutano wa wanachama wa CUF ambao wanamuunga mkono, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na kuwapiga wanachama wa CUF pamoja na waandishi wa habari ambao walikuwepo eneo hilo. 

Mkutano huo ambao ulikuwa na lengo la kumtambulisha Katibu Mkuu wa CUF , ulivurugika baada ya vurugu kubwa zinazodaiwa kufanywa na wanachama wa CUf ambao wanamuunga mkono Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba. 

katika vurugu hizo, Mtu mmoja ambaye bado hajafahamika jina lake miongoni mwa waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu kutoroka.
Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la uvamizi wa Mkutano wa wanachama wa CUF uliotokea mwishoni mwa wiki hii. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...