Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi amefanya ukaguzi wa mfumo wa kodi ya
ardhi katika manispaa ya Musoma Mjini mkoa wa Mara ambapo amebaini wananchi 231
wanadaiwa Kodi ya Pango la Ardhi kiasi cha shilingi milioni 271.
Mhe Lukuvi amemtaka
Afisa Ardhi wa manispaa ya Musoma bwana Joseph Kamonga kuwasilisha majina ya
wadaiwa hao katika Mahakama ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni
pamoja na kupiga mnada majengo na mali zao kawa wakikaidi kulipa kodi hiyo.
“Nimeagiza kesi za
madai ya kodi zitolewe hukumu ndani ya siku moja tu ili wadaiwa waweze
kuchukuliwa hatua ya kuuzwa kwa mali zao haraka” Mhe Lukuvi aliyasema hayo
wakati alipo fanya ziara ya kukagua mfumo wa kodi wa manispaa ya Musoma mjini
ili kuhakikisha wamiliki wote wa ardhi nchini wanalipa kodi kwa hiari kabla ya
hatua za kisheria hazijafuata dhidi yao.
Aidha, Waziri Lukuvi
amefanya uzinduzi wa mpango kabambe (Master Plan) wa Manispaa ya Musoma na
kuwapongeza viongozi na watendaji wa manispaa ya Musoma kwa kuwa manispaa ya
kwanza nchini kuweza kuzindua mpango kabambe wa mji wao. Pia aliwapongeza kwa
uzalendo wao wa kutumia kampuni za ndani katika utekelezaji wa mpango huo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mh. William Lukuvi akikagua mfumo wa kodi wa Manispaa ya Musoma Mkoani
Mara. Kushoto kwake Afirsa Ardhi wa Manispaa hiyo Ndugu Joseph Kamonga
akimuonesha mfumo wa kodi unavyofanya kazi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mh. William Lukuvi akikambidhi Mpango Kabambe wa Manispaa ya Musoma Meya
wa Manispaa ya hiyo Mh. Patrick Gumbo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mh. William Lukuvi akizindua Mpango Kabambe (Master Plan) Manispaa ya
Musoma Mkoani Mara.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mh. William Lukuvi akiongea na viongozi na wananchi wa Manispaa ya
Musoma katika uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Manispaa hiyo.
Baadhi ya Wananchi na Watendaji wa
Manispaa ya Musoma wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mh. William Lukuvi katika uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Manispaa hiyo mkoani
mara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...