WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa mashuleni waendelee na masomo yao ili kufikia malengo walioyanayo nchini.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa maswala ya kijinsia ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri8 ya Muungano waq Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo jijini Dar es salaam.

“Tunapokataza watoto wa kike wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa mashuleni tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao kwa wakati waliotarajia”alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa anaunga mkono uamuzi wa Rais wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli kwa kutoa elimu bure nchini kwani kunaongeza idadi ya watoto wa kike kuwepo mashuleni tofauti na kipindi cha nyuma.

Mbali na hayo Waziri Ummy ametoa wito kwa wazazi kuwahamasisha watoto wao wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kukuza rasilimali watu katika kujenga uchumi unaotokana na viwanda nchini.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha DUCE Prof. William Anangisye amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuleta chachu ya kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kupata wanasayansi wanawake nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akimuwakilisha Makamu wa Raisi Bi Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Masuala ya Usawa wakijinsia ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE) jijini Dar Es salaam.
Prof Rwekaza Mukandala Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar Es Salaam akihutubia wadau na wanafunzi waliojitokeza katika mkutano wa kwanza wa masuala ya Jinsia na Usawa yaliyofanyika katika chuo kikuu cha Uwalimu DUCE jijini Dar Es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha DUCE Prof. William Anangisye akihutubia jopo la Wadau na wanafunzi katika mkutano wa masuala ya Usawa na huku akisisitiza wazazi na walezi kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kupata wanasayansi wanawake nchini.
Wadau wa Masuala ya Usawa wa kijinsia wakifuatilia kwa ukaribu ujumbe uliokuwa ukitolewa na Mh.Ummy Mwalimu Waziri wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto aliyekuwa akimuwakilisha Makamu wa Raisi Bi Samia Suluhu Hassan katika viunga vya Chuo cha Uwalimu DUCE jijini Dar Es Salaam.
Picha ya pamoja ya wadau wa masuala ya Usawa wakijinsia katika mkutano wa kwanza wa masuala ya Usawa wakijinsia uliowakutanisha kujadili na kuhamasisha juu ya kumlinda mtoto wa kike ili apate Elimu sawa kama ile apatayo mtoto wakiume katika jamii yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...