Suala la uhaba wa vitabu vya masomo ya Sayansi, maabara pamoja na walimu wa masomo hayo limekuwa likisababisha baadhi ya wananfunzi kushindwa kumudu na hivyo kuyaepuka masomo hayo,licha ya serikali na wadau mbalimbali kuhamasisha wanafunzi kuchukua masomo hayo.

Kutokana na hali hiyo Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel imetoa msaada wa Vitabu vya Masomo ya Sayansi vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tatu katika Shule ya Sekondari Vianzi iliyopo  Mkuranga Mkoani Pwani ambayo ina zaidi ya wanafunzi 400 ikiwa na walimu watatu kwa masomo yote ya Sayansi (biolojia, fizikia, kemia na hesabu). Hatua hiyo ni mwendelezo wa Kampuni  hiyo kusaidia katika elimu shule mbalimbali hapa nchini ili kuinua kiwango cha elimu katika masomo ya Sayansi.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Vianzi Mwl. Ashura Manaki amesema kuwa shule yake imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu, maabara za kutosha pamoja na vitabu hali ambayo imekuwa ikisababisha wanafunzi kukimbia masomo ya Sayansi.
“Tunaishukuru sana Airtel kwa msaada huu wa vitabu ebu fikilia tuna upungufu wa walimu,sasa likija tatizo la ukosefu wa vitabu unadhani wanafunzi watayapenda masomo ya sayansi,lakini kwa sasa nina matumaini tutaweza kusonga mbele,”alisema Manaki.

Kwa upande wa Meneja wa Huduma kwa Jamii kutoka Airtel Hawa Bayumi ameleeza kuwa licha ya Kampuni hiyo kujikita katika mambo mbalimbali ya Kijamii wameona umuhimu wa kuisaidia shule hiyo ambayo inachangamoto ya walimu wa sayansi lakini wakakuta hata vitabu navyo ni changamoto wakaamua kutoa msaadahuo.

”Licha ya Airtel kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii tumeona kuna umuhimu mkubwa kuisaidia vitabu vya sayansi shule hii kutokana na kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu wa sayansi pamoja na vitabu vya sayansi tuna matumaini vitaweza kusaidia shule hii kujenga wataalamu wa sayansi hasa ukizingatia serikali inaweka juhudi kufikia Tanzania ya viwanda ni muhimu kuwekeza katika rasilimali watu na kujenga watanzania weny weledi. Lengo letu ni kuendelea kuwezesha vijana kufikia malengo yao kupitie elimu na ujasiriamali,”alisema Bayumi.

Zamda Said ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo amesema kuwa shule hiyo bado ina mahitaji ya walimu wa sayansi lakini kwa kupatiwa vitabu hivyo vitasadia hata wanafunzi kuweza kujisomea huku akiwaasa wanafunzi kutumia fursa hiyo kufaulu masomo ya sayansi.

“Ni kweli tatizo la uhaba wa walimu pamoja na ukosefu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia ni changamoto kwa shule hii lakini nawaombeni wanafunzi kutumia fursa hii kuweza kujisomea maana vitabu gharama yake ni kubwa,”alisema Said.
Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi akimkabidhi vitabu vya sayansi, Maria Edward, mwanafunzi wa Shule ya sekondari ya Vianzi iliyopo Mkuranga wakati Airtel ilipotembelea shule hiyo kutoa msaada wa vitabu vya taaluma .
Mkuu wa shule ya Shule ya sekondari ya Vianzi Ashura Manaki ( wa pili kulia ) kaifatiwa na pamoja na Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi (wapili kushoto) na Meneja Mauzo wa Airtel Pwani, Philipi Nkupuma kwa pamoja wakionyesha vitabu vya sayansi mara baada ya Airtel kukabidhi vitabu hivyo kwa shule ya sekondari ya Vianzi pindi walipotembelea shuleni hapo.
Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi akimkabidhi vitabu vya sayansi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Vianzi Bi Ashura Manaki wakati Airtel ilipotembelea shule hiyo kutoa msaada wa vitabu vya taaluma . akishuhusia ni Zamda Said ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...