MAONESHO ya Vyuo Vikuu vya nchini India yanatarajiwa kufanyika kesho huku yakitarajiwa kutoa fursa kwa wanafunzi wa Kitanzania kuvifahamu vyuo vilivyopo nchini humo na ubora wa taaluma zake.

Maonesho hayo ambayo yameandaliwa na Global Education Link (GEL) kwa kushirikiana na Ubalozi wa India nchini yatafanyika kesho katika ubalozi huo uliopo jirani na Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).

Akizungumzia maonesho hayo, Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel amesema, wanafunzi wa kitanzania wamekuwa wakikumbana na changamoto kubwa ya kudsoma katika vyuo ambavyo havina ifa.

“Unakuta mwanafunzi anapewa taarifa ambazo si sahihi hata katika vyuo anachokwenda, na ndio sababu tumeamua kuandaa maonesho hayo ili kubaini vyuo sahihi,” alisema.

Amesema wanafunzo wengi wamejikuta wakisoma katika vyuo ambavyo havina hadhi sawa na ile waliyotegemea, hatua inayowawia vigumu katika kutambulika na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU).

Kwa upande wake Balozi wa India nchini, Sandeep Arya amesema maonesho hayo yatafanyika Kesho na keshokutwa katika ubalozi wa India na kwamba lengo kubwa ni kuwaunganisha wanafunzi wa kitanzania wanaolenga kusoma katika nchi hiyo na vyuo vyenye ubora.

Arya amesema maonesho hayo yatashirikisha taasisi 20 za vyuo vikuu ambazo zinazotoa fani tofauti katika ngazi zote za elimu ya juu.

01.Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel akizungumzia juu ya maonesho hayo ya Vyuo Vikuu vya nchini India yanatarajiwa kufanyika kesho katika ubalozi huo uliopo jirani na Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...