Serikali imeitaka Bodi ya Chuo Cha Bahari Dar es Salaam (DMI), kuhakikisha inaboresha miundombinu ya chuo na kuzingatia miiko na kanuni za ufundishaji ili wanafunzi wanaohitimu chuoni hapo waweze kukidhi mahitaji ya soko.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati akizindua bodi hiyo na kusisitiza kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha majengo kwa kutangaza zabuni kwa uwazi ili kuepuka mianya ya rushwa.

“Hakikisheni mnakuwa na mpango madubuti wa kuboresha majengo ya chuo ili chuo kibaki na hadhi yake, lakini pia hakikisheni mntoa elimu bora kwa wanafunzi wanaokuja kusoma hapa ili waweze kupata misingi imara itakayowawezesha kuajiriwa ndani na nje ya nchi mara baada ya kuhitimu masomo yao”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa Serikali ina uhitaji wa wataalam wengi kwenye masuala ya bahari hivyo ni wajibu wa bodi kusimamia chuo na kuhakikisha wataalam hao wanazalishwa kwa wingi chuoni hapo ili kukidhi mahitaji ya soko kitaifa na kimataifa.

Amewataka wakufunzi wa chuo hicho kuhakikisha wanatumia lugha nzuri kwenye ufundishaji ili kuwaweka wanafunzi karibu na kuhakikisha wanapata taaluma inayotakiwa kwani kuwepo kwa waalimu hao kunategemea kuwepo kwa wanafunzi.

“Ni lazima tufungue milango kwa wanafunzi sababu wapo wanaoelewa haraka na wanaoelewa taratibu, hivyo tukae nao muda mrefu ili kubaini changamoto zao lakini pia tuwe waangalifu juu ya matumizi ya lugha tunazotumia kwa wanafunzi wakati tunapofundisha”, amefafanua Prof. Mbarawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...