NI BAADA YA WAKULIMA 18 KUKAIDI AGIZO LA WAZIRI MKUU.
·        ATAKAYEKAMATWA TUMBAKU YAKE KUTAIFISHWA
 
Na Tiganya Vincent
 RS-Tabora

 
Mkuu wa  Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri amepiga marufuku usafirishaji wa  tumbaku kutoka Wilaya moja kwenda nyingine ili kudhibiti utoroshaji unaotarajiwa kufanya na baadhi ya wakulima wasio waaminifu ambao hadi hivi sasa wamekaidi agizo la Waziri Mkuu la kuwataka wakulima wote kuuza  tumbaku yao kupitia Vyama vya Msingi vilivyopo katika maeneo yao.
 
Marufuku hiyo inafuatia wakulima wa kujitegemea (IF) zaidi ya 16 kutoka Wilaya ya Urambo na Uyui kukataa kujisajili katika Vyama vya Msingi na hivyo kutoonyesha kuwa watauzia tumbaku yao kupitia  Chama gani cha Msingi.
 
Mkuu wa Mkoa huyo alitoa agizo hilo jana mjini Tabora wakati wa kikao cha wadau wa tumbaku, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , ambapo pamoja na mambo mengine kupitia Bodi ya Tumbaku Tanzania kimejadili tarehe ya kuanza kwa  masoko ya tumbaku ambayo yataanza siku ya Ijumaa wiki hii (26.5.2017) katika meneo mbalimbali.
 
Alisema kuwa Serikali iliamua wakulima wote kuuzia tumbaku yao kupitia Vyama vya Msingi katika maeneo yao na sio vinginevyo ili kuepuka watu wanatumia mwanya wa kujitegemea kuwarubuni  tumbaku ya wakulima wadogo wadogo walipo katika vyama vya msingi na kuwauzia baadhi ya tumbaku yao na kusababisha madeni katika vyama vyao vya Msingi.
 
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa hadi hivi sasa baadhi ya wakulima hao wamekata kujisajili katika Vyama vya Msingi vilivyopo katika maeneo yao na hata kwingine ni ishara tosha kuwa wanampango wa kutorosha tumbaku hiyo kwenda kuuzia wanakujua kinyume na agizo la Waziri Mkuu.
 
Alisisitiza kuwa yeye akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa , hawezi kukubali watu wakaidi agizo la Waziri Mkuu kwa nia ya kutaka kuwanyonya wakulima wengine.
 
Kufuatia hali hiyo aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , Wilaya kushirikiana na Watendaji ngazi za chini na kuwakamata wao na mizigo yote itakayokuwa inasafirisha nje ya eneo la Chama cha Msingi la Mkulima anapokaa kama bidhaa hiyo haijanunuliwa na kupata hati inayotambulika na Bodi ya Tumbaku ya Tanzania (TTB) na wanunuzi rasmi wa tumbaku wenye vibali vya kufanya kazi hiyo mkoani Tabora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...