Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi katika kipindi cha mwaka 2010-2015 imekamata   vyombo 2795,injini za Mitumbwi 118,magari 297 na pikipiki 33 kwa sababu ya uvuvi haramu na utoroshwaji haramu kupitia  maziwa makubwa,mwambao wa Bahari ya Hindi na Mipaka ya Nchi.
Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Fakharia Khamis.
“Katika kukabiliana na wavuvi haramu,Wizara imeanzisha na kuimarisha vituo 25 vya Doria kwenye Maziwa makuu,Mwambao wa Bahari ya Hindi na mipaka ya nchi”Alisema Mhe.Ole Nasha.
Aidha amesema kuwa kuwepo kwa vituo hivyo kumeongeza uwezo wa kukabiliana na uvuvi na biashara haramu kupitia operesheni mbalimbali  ambapo pamoja na jitihada za Serikali tatizo hili bado linaitaji mkazo mkubwa sana katika maneo ya mialo na masoko.
Aidha Serikali imeanzisha kikosi kazi cha Kitaifa Mult Agency Task Team (MATT) ambacho kinafanya kazi ya kudhibiti uhalifu wa mazingira ikiwemo kudhibiti uvuvi haramu hususan matumizi ya mabomu katika shughuli za uvuvi uku pia Maboresho ya Sera,Sheria,na Kanuni za Uvuvi zikifanyiwa kazi ili kuimarisha usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi nchini.
Kwa upande mwingine katika kipindi hicho cha 2010-2015 watuhumiwa 3792 walikamatwa na kesi 243 zilifunguliwa mahakamani ambapo pia jumla ya  shilingi 158,559,323 zilikusanywa ikiwa ni faini kutokana na makosa mbalimbali uku watuhumiwa 11 wakifungwa.
Mhe.Ole Nasha pia alitoa wito kwa wabunge ambao ni wajumbe katika halmashauri waendelee kutoa elimu kwa wavuvi kuhusu madhara ya uvuvi haramu, na kuhimiza Halmshauri zao katika kudhibiti uvuvi haramu kwenye maeneo yao.

“Naziomba Jamii za Wavuvi na wadau wote washirikishwe katika kusimamia rasilimali za uvuvi na matumizi endelevu kwa ajili ya kuwapatia wananchi ajira,chakula na uchumi wao na Taifa kwa ujumla ili kudhibiti uvuvi haramu”Alisisitiza Mhe.Ole Nasha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...