Na Tiganya Vincent, Sikonge 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ameteua timu ya Maafisa watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa ajili ya kuandaa taarifa(ripoti) itakayowasilishwa kwake Jumatano(wiki inayoanza kesho) ili imwezeshe kutoa maamuzi yatakaondoa kuondoa mgogoro uliosababisha ujenzi Mradi wa Bwawa la Umwagiliaji la Uluwa ushindwe kuendelea kwa sababu ya maji yake kuelekezwa katika Msitu wa Hifadhi wa Ipembampazi. 

Hatua hiyo itasaidia kuokoa zaidi ya shilingi milioni 313 ambazo hadi hivi sasa zimeshatumika katika ujenzi wa mradi huo ambao ni kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa mpunga katika vijiji viwili vya Mtakuja na Kiloleni kama mradi utaendelea. Profesa Maghembe alichukua uamuzi huyo jana wilayani Sikonge baada ya kutembelea Mradi huo huku akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ili kujionea hatua ulipokuwa umefikia na hiyo mifereji ilijengwa kuelekea katika Msitu wa Hifadhi. 

Alistaja wataalam hao kuwa ni Ofisa wa Maliasili, Misitu, Kilimo na Mhandisi wa Maji, Mhandishi wa Ujenzi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mteandaji wa Halmashauri ya Sikonge ambao aliwapa jukumu la kuandaa taarifa itakayoonyesha mambo mbalimbali ikiwemo kupima na kuonyesha kiasi cha eneo ambalo wananchi wanalohitaji kwa ajili ya kilimo hicho na eneo lilobaki katika Msitu huo wa Hifadhi. 

Profesa Maghembe aliwaambia kuwa uharaka na ubora wa ripoti ya Halmashauri ndio utakaoisaidi Wizara ya Maliasili na Utalii kufikia maamuzi haraka ambayo baada ya wataalam wake kuipitia atawalisha mapendekezo na hatua waliofikia kwa Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya hatua zaidi. 

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...