Vijana kutoka mataifa mbalimbali waliokusanyika katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN), mjini Arusha wametakiwa kuchambua masuala yaliyopo mbele yao kwa makini ili kutoa jawabu kwa matatizo ya dunia yanayohitaji ushiriki wao.

 Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa serikali katika mkutano huo Ngusekela Karen Nyerere, Ofisa anayeshughulikia dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Aliwataka vijana wanaoshiriki TIMUN kuhakikisha wanaangalia kwa makini mambo yanayogusa nchi zao na kuyatafutia ufumbuzi kwa kuwa ndio njia pekee ya kutekeleza malengo endelevu ya dunia ambayo yanahitaji ushirikiano wa ndani na wa kimataifa. TIMUN ambayo kirefu chake ni Tanzania International Model United Nations hufanyika kila mwaka na ujumbe mbalimbali na mwaka huu ujumbe wa TIMUN ni: “kuwawezesha vijana katika diplomasia na uongozi” Picha juu na chini ni Ofisa wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) unaofanyika kwenye Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) mjini Arusha.

TIMUN huandaliwa na Shirikisho la vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) taasisi ya vijana isiyotengeneza faida inayotangaza shughuli za Umoja wa Mataifa na kushirikisha vijana katika utekelezaji wa shughuli hizo. 

Aidha aliwashukuru waandazi wa mkutano huo kubwa unaofanana na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (General Assembly) wenye lengo la kukutanisha vijana kujadili mustakabali wa malengo ya dunia. 

Alisema vijana wana nafasi muhimu katika utekelezaji wa malengo hayo ya maendeleo endelevu jukumu ambalo dunia imejipa kwa miaka 15 hadi mwaka 2030. Pamoja na kuwashukuru Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST) kwa kukubali kuwa mwenyeji wa kambi hiyo, hali iliyoonesha kwamba wanajali vijana, mwakilishi huyo wa serikali alisema kwamba Tanzania ipo tayari kusukuma mbele ajenda ya ushirikishaji vijana katika maendeleo endelevu kwa kuwa inaamini juu ya hilo. “Wakati serikali inafanyakazi kwa karibu na taasisi nyingine kuhakikisha kwamba malengo ya maendeleo yanatekelezeka, baraza la vijana ambalo litakutana litakuwa na kazi kubwa ya kutengeneza sauti ya pamoja namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo” Alisema kwamba malengo ya dunia ambayo yapo 17 yanagusa kila sehemu ya maisha na hivyo ni vyema kama vijana watatoka na majibu ya maswali yanaoumiza vichwa kuhusu malengo hayo hasa mazingira na dunia endelevu. 

Aliwataka vijana kutumia nafasi yao vyema katika jukwaa hilo kwani maisha ya watu bilioni 7 duniani wanategemea namna ambavyo wanajengwa na vijana, wenye mchango muhimu wa kulinda mazingira na kuhakikisha maendeleo endelevu. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017), unaofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) mjini Arusha.

Awali Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kwamba zaidi ya vijana elfu 20 nchini Tanzania wamefunzwa malengo endelevu ya dunia, toka ulipofanyika uzinduzi Juni, 2016. 

Akizungumza katika hafla ya kambi ya mwaka huu ya Tanzania International Model United Nations (TIMUN), inayofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST), Bw. Rodriguez alielezea kufurahishwa na idadi hiyo ya vijana waliohamasishwa na kusema kwamba malengo ya maendeleo endelevu 2030 yanahitaji kila mmoja kushiriki. Aidha alielezea umuhimu wa ushiriki wa vijana katika masuala ya maendeleo kutokana na uwingi wao hapa nchini. Asilimia 67 ya watu nchini ni vijana. Mkutano ukiendelea katika ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) jijini Arusha. Bw. Rodriguez alishukuru machampioni kwa kuwezesha vijana wenzao kutambua malengo endelevu ya dunia na kuwataka kuendelea kufanya vizuri zaidi katika kuwashawishi vijana wenzao kuelewa na kushiriki katika malengo hayo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...