Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2017/2018 leo  mjini Dodoma. UNAWEZA KUSOMA HOTUBA ALIYOIWASILISHA HAPO CHINI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. MH.WAZIRI BWA.MAGEMBE ACHA KUPOTOSHA WATANZANIA HUWEZI KUWADHULUMU WATANZANIA HAWA KWA KUWAONGEZEA UMASIKINI NIJAMBO LA KUSIKITISHA SANA NA HII INAFANYA WATANZANIA MILIONI MOJA WAIONE HII SERIKALI YA AWAMU YA TANO NI MBAYA AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA KATIKA MAISHA YAO.NI JAMBO LA KUSIKITISHA NA KWA KUWAINGIZA KATIKA UMASIKINI WAFANYABIASHARA WA VIUMBE HAI,UNACHOONGEA HAPO UNAPOTOSHA HAKUNA UKWELI WOWOTE KUTHIBITISHA KUNA UKIUKWAJI WA TARATIBU,NASHANGAA WABUNGE WA TANZANIA KUTOTETEA AU KUJUA UKWELI WA SUALA HILI.HII NI DHAMBI KWA MUNGU KWA SERIKALI HII YA AWAMU YA TANO ILICHOTUFANYIA HATA HAKI ZA BINADAMU ZIMEKIUKWA HAZIPO,HUWEZI KWENDA KUSIMAMISHA BIASHARA GHAFLA WAKATI WATU WAMELIPIA VIBALI WANA VIUMBE HAI WANAMASHAMBA AMBAYO KWA MABILIONI YA SHILINGI WAMEIINVEST KWA ZAIDI YA MIAKA 35,WATALISHA NINI HAWA VIUMBE IKIWA HAWAWEZI KUUZA NJE WANACHOZALISHA KATIKA MASHAMBA,RANCHI ZAO.HII NI MBAYA SANA NA HAIJAWAHI TOKEA TANGU UHURU NDIYO MAANA HAWA WAFANYABIASHARA WANATAKA KUKUTANA NA RAIS WAELEZE UKWELI NA WEWE UWEPO HUU NI UONEVU MKUBWA KWA WATANZANIA HAWA NI JAMBO LINALOUMA SANA NA KUSIKITISHA,WATU WANA MIKOPO KATIKA MABENKI,SACCOS,NK WAMEPOTEZA HAKI NA MALI ZAO WAZIRI HUYU HAFAI,KABISA NI MTU MBAYA AMBAYE ANAFANYA WATANZANIA HAWA WAIONE SERIKALI HII NI MBAYA ISYOJALI WAFANYA BIASHARA HAWA VIUMBE HAI WALIOLIPA PESA ZAO,VIUMBE,HEATH CERTIFICATES,FREIGHT CHARGES KWENYE AIRLINES NA KUWA NA VIBALI HALALI EEEEEEEEEEEEE MUNGU NAOMBA UTUSIKIE !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Mh. Pro. Jumanne Magembe.
    Kwa kweli hotuba yako ulioitoa leo Bungeni kuhusu kufunga biashara ya kusafirisha viumbe hai pori nje ya nchi, hii ni dhahiri umeonyesha ni jinsi gani hauko makini katika kuchambua mambo muhimu na kuyafanyia kazi hatimaye kuyatolea maamuzi kwa manufaa ya watanzania na Taifa kwa ujumla.

    Kwa mujibu wa Sheria,taratibu na kanuni za uhifadhi wa wanyamapori umekiuka usimamizi bora juu ya uhifadhi.

    Mnamo mwezi March, 2016 ulisitisha usafirishaji viumbe hai pori nje ya nchi bila kushirikisha wataalam wako na hata wafanyabiashara wa viumbe hai pori, hii ni ukiukwaji wa usimamizi bora wa uhifadhi wa viumbe pori hai na hata kiutawala,kwani maamuzi yako yameleta matatizo makubwa na hasara kwa wafanya biashara hawa na hata kwa Taifa kwa ujumla, kwani kutamka kulipa fidia ina maanisha unakiri kutokuwepo na kosa lolote lililofanywa na hawa wafanya biashara.

    Ifahamike kuwa kila mwaka Wizara yako ya Maliasili na utalii hutoa Leseni kwa wafanya biashara wa viumbe hai pori baada ya kukidhi vigezo. Kwa mantiki hiyo, ina maana wafanya biashara hawa watanzania waliingia mkataba na Serikali yao ili waweze kupatia huduma halali ikiwa ni pamoja na kukatia Leseni,vibali vyote muhimu, kukamata viumbe hao, kuwasafirisha hadi kwenye mazizi yao,na pia kuwapa huduma zingine muhimu kama, kuwalisha, kuwatibu na kupata huduma zingine za hati zinazothibibitisha afya ya viumbe hao kupitia Wizaara ya kilimo na mifugo kitengo cha (Veternary)

    Kitendo cha kusitisha biasshara hiyo ghafla hukuzingatia maslahi ya wafanyabiashara hawa na Taifa kwa ujumla. Hii inathibitisha kwamba hukuwa makini katika maamuzi yako kwani hata hizo fedha unazodai kuwalipa hawa wafanya biashara takriban Tz sh.3.6 billion,utazipata wapi wakati hata watanzania wengine huko Serengeti vijijini waliopatwa na mashambulio ya wanyamapori tangu mwaka 2005 hadi leo hawajalipwa. Je, wewe Magembe utatoa fedha hizi wapi?? wakati Serikali ya awamu ya tano inasisitiza kukusanya mapato kwa maendeleo ya watanzania??

    Ulitakiwa kujua kuwa hawa viumbe pori hai wanapatikana maeneo ya WAZI TU na si kwenye maeneo ya HIFADHI ZA TAIFA, kwa maana nyingine ni kwamba hakuna njia mbadala wa matumizi ya viumbe pori hawa zaidi ya kuangamizwa wakati shughuli mbalimbali za maendeleo yayakifanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Ni ukweli kwamba hutakuwa na marekebisho yoyote muhimu zaidi ya utaratibu uliokuwepo awali.

    Unatakiwa kujua na kuishauri serikali matumizi bora ya viumbe pori hawa. Kuwa, kabla ya kuangamizwa viumbe hawa kwa kutumia gharama kubwa ya fedha za walipa kodi, basi watanzania wafanyabiashara hawa wakepewa fursa ya kuwatumia viumbe pori hawa kwa kuwageuza kuwa rasilimali na hivyo wakaweza kujiajiri na kujipatia mapato na kuweza kuendeleza maisha yao na pia Serikali ikaweza kujipatia mapato kwa kukusanya mirahaba.

    ReplyDelete
  3. Mh. Magembe ameonyesha hajui chochote kuhusiana na hii biashara ya viumbe hai au amehamua Kwa makusudi kabisa kudanganya bunge juu ya ukamatwaji Wa wanyama hai , wanyama wengi wanaokusanywa wanatoka katika maeneo ya wazi sio kwenye mapori tengefu y hifadhi , ata wasipokusanywa na kuuzwa automatically watauwawa na binadamu, hapo kama kweli una PhD iliitaji kujua faida na hasara ya kufunga hii biashara? Umewaacha wafanya biashara wengi hawana pa kushika tena , fidia haitowasaidia watu ambao wameshachukua advance payment za wateja wao na mzigo haukuenda, unafikiri umetengeneza nini kati ya mteja na mfanya biashara? Wabunge hii ndio sehemu yenu ya kuwapigania wananchi wenu na kubainisha uongo Wa mtu mmoja serikalini na kuipaka tope serikali.

    ReplyDelete
  4. Tatizo jingine kubwa ni kuwa viongozi serikali hii hawataki kuwasikiliza watu hawa.mfano waziri mkuu tangu june 2016 mpaka hii leo haoni umuhimu wa kuwasikiliza wataabika hawa.zaidi ya kupata shida ya kutafuta nafasi ya kumwona kuwa shidaaaaaaaa,huku watu wakiendelea kataabika kwa mateso makubwa ya kuhudumia viumbe hawa ambao wanaendelea kufa tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...