BENKI ya Diamond Trust(DTB) Tawi la Tanga wanakusudia kupanua wigo wa huduma zao kwa wateja kwa kukarabati na kuongeza namba ya wahudumu ikiwa ni mkakakti wa ujio wa fursa mbalimbali mkoani hapa ukiwemo mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Hayo yalibainishwa juzi na Meneja wa Benki ya Diamond Trust Bank Mkoani Tanga (DTB) Athumani Juhudi wakati futari iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wateja wao wa mkoa wa Tanga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Tanga Beach Resort mjini hapa na kuhu dhuiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za Handeni na Tanga.
Alisema wao wanakusudia kufanya hivyo ili kuweza kuendana na wigo mpana wa ukuaji wa uchumi kwa mkoa wa Tanga ambao unatarajiwa kufanyika kutokana na mradi huo mkubwa .
“Benki yetu ipo kwenye nafasi ya tano kati ya mabenki zenye amana kubwa za wateja hivyo tumeona kuwaandalia futari hiyo ni namna bora ya kuwashukuru wao kwa kuwasapoti”Alisema.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya DTB kwa ajili ya wateja wao mkoani Tanga  iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort,kulia ni Shehe wa Mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu na kushoto ni Meneja wa Benki ya DTB Mkoani Tanga,Athumani Juhudi
 MKUU wa wilaya ya Tanga,Thobias mwilapwa akizungumza wakati wa futari hiyo
 Shehe wa Mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu akitoa neno kwenye futari hiyo
 Meneja wa Benki ya Diamond Trust Bank Mkoani Tanga (DTB) Athumani Juhudi akizungumza na waandishi wa habari.
Kwa habari kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...