Hivi ndivyo Ufukwe wa Coco (Coo Beach) ulivyofurika watu wa aina mbalimbali hapo jana jioni, katika kusherehekea sikukuu ya Iddi pili,Mabasi/Daladala kutoka kona kadhaa za jiji la Dar zilionekana zikishusha watu kwa wingi katika ufukwe huo ambao ulisheheni pia vyakula vya kila aina ikiwemo Mihogo,Chips mayai na wengine walikutwa na Camera ya Blogu ya jamii wakiwa wemebeba vyakula vyao na kujibweda kando kando ya ufukwe,ama kwa hakika ilikuwa burudani kwa wakazi wa jiji la Dar.Picha na Michuzi Jr.

Kuhakikisha ulinzi na usalama wa kutosha unakuwepo,Jeshi la Polsi lilipiga kambi kabisa eneo hilo,kwa idadi ya watu ilikuwa ni kubwa.
Sehemu za kupaki magari zikaonekana hazitoshi kabisa
Foleni ya kuingia kando kando ya ufukwe nayo ilikuwa kubwa kiasi ambacho magari mengine yalipita kwa taabu kuendelea na safari zake.
Chopa ya Jeshi la polisi nayo ilikuwa na kazi ya ziada kama hivi ya kukagua meneo mbalimbali yaliyokuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu,Pichani chini Chopa ikionekana kwa mbali ilipokuwa ikikatiza maeneo hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...