Mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo akikabidhi misaada kwa Mwenyekiti wa Taasisi inayoshughulikia masuala mbalimbali ya Wajane na Watoto Yatima ijulikanayo kwa jina la Ahbaabul Khairiya, Ahmed Chebe ya Mwanayamala B jijini Dar es Salaam. Jokate ambaye pia ni Kaimu Katibu Hamasa na Chipukizi wa Umoja wa Vijana Tanzania (UVCCM) amebidhi kilo 250 za unga na mchele, mbuzi wawili, mafuta ya kupikia, nguo za watoto wa kike na wa kiume, mafuta yakupikia na nguo za watu wazima kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwa faraja zaidi.

Mwanamitindo, Miss Tanzania namba mbili 2006 na mbunifu wa mavazi, Jokate Mwegelo ametoa sadaka ya sikukuu ya Eid El Fitr kwa taasisi ya wanawake wajane na watoto yatima ilijulikanayo kwa jina la Ahbaabul Khairiya cha Mwanayamala B jijini Dar es Salaam. Jokate ametoa zawadi hiyo kwa kituo hicho chenye jumla ya wajane 32 na watoto yatima 41 kama sehemu ya kuwafanya wajane na yatima hao kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwa faraja zaidi.

Mrembo huyo ambaye pia ni Kaimu Katibu Hamasa na Chipukizi wa Umoja wa Vijana Tanzania (UVCCM) amebidhi kilo 250 za unga na mchele, Mbuzi wawili, mafuta ya kupikia, nguo za watoto wa kike na wa kiume, mafuta yakupikia na  nguo za watu wazima.

Amesema kuwa ameguswa na changamoto za kituo hicho ambacho kimefanya kazi kubwa kujua changamoto mbalimbali za wajane na watoto yatima wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

“Nimegushwa sana na kuamua kidogo nilichonacho kugawana na ninyi, sikukuu ya Eid El Fitr inakaribia na natarajia kila mmoja wetu atasheherekea kwa faraja zaidi, naomba mpokee msaada huu na matarajio yangu ni kuendelea kuwasaidia pindi ninapata nafasi,” alisema Jokate.

Mmoja wa wasanii wa luninga nchini, Juma Chikoka ambaye alikuwa katika makabidhiano hayo alitoa wito kwa jamii kuunga mkono juhudi za Jokate za kutatua changamoto mbalimbali katika jamii. Mwenyekiti (Amiri) wa Taasisi hiyo, Ahmed Shebe alimshukuru Jokate kwa msaada huo na kuomba wadau mbalimbali kujitokeza kutatua changamoto hizo.

“Taasisi inahudumia wajane wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, wapo wengine Chalinze na Bagamoyo mbali ya hapa wa jijini, tunajitahidi kutafuta michango sehemu mbalimbali ili kuweza kuondoa changamoto hizi, hata hivyo bado hatujafikia lengo, tunahitaji msaada kwa wasamaria ili kuwapa faraja zaidi,”

“Kuna wajane wanaosaidiwa kulipia kodi yay a nyumba na watoto yatima wanaolipiwa ada, hatuna uwezo mkubwa wa kufanya hivyo na zaidi fedha za msaada zinatokana na michango yetu,” alsema Shebe.
Mmoja wa wajane wa Taasisi ya Ahbaabul Khairiya, Nawili Saidi akibeba nguo mbalimbali zilizotolewa na Mwanamitindo, Jokate Mwegelo kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr.
Jokate akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kituo cha Ahbaabul Khairiya pamoja na wajane na yatima.
Wanawake wajane wakimshukuru Jokate mara baada ya kutoa msaada katika kituo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...