Wakati uhalifu wa mtandao ukionekana kushika kasi duniani, Jamii imetakiwa kuzitumia simu za mkononi katika kulisaidia jeshi la polisi kubainisha watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kama sehemu ya kutekeleza haki yao ya kikatiba

Wito huo ulitolewa na Mkaguzi wa Polisi Merkiad Makumba jana kwa niaba ya Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Korogwe , wakati akizindua duka la Kisasa la kampuni ya simu za mkononi la Airtel katika wilaya hiyo mkoani Tanga. Hatua hiyo itasaidia kukabiliana na vitendo vya namna hiyo ambavyo vinahatarisha ustawi wa raia na mali zao…alisema Mkaguzi Makumba.

“ Wahalifu wengi wanatumia mawasiliano ya simu za mkononi na wamekuwa wakiwasiliana nanyi,iwapo mtazitumia simu kwa nia njema Tanzania itakuwa sehemu salama ya kuishi” alisema Mkaguzi Mkumba. Meneja mauzo wa Airtel Tang, Habibu Kiango alisema duka hilo limewarahisishia wateja kupata huduma za Airtel kwa urahisi zaidi blia ya kwenda umbali mrefu kufuata huduma za mawasiliano . natoa wito kwa wakazi wa hapa na maeneo ya karibu kutumia fursa hii katika kukuza na kuendeleza biashara zao.

Kiango aliongeza kwa kusema duka hili litatoa huduma nyingi pamoja na kusajili line, kutoa huduma za kifedha za Airtel Money, kuunganisha wateja na huduma za intaneti na nyingine nyingi , aidha alitumia fursa hilo kuwakaribisha wakazi wa Korogwe kulitembelea duka hilo.

Mpaka sasa Airtel imeshazindua maduka mengine kama hili katika mikoa ya Shinyanga, Dodoma, Arusha , Manyara , Dar na Morogoro. Mpango huo wa kuzindua maduka ya kutoa hudma kwa wateja unalenga kupanua na kusogeza huduma za AIRTEL karibu na jamii hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma hizi muhimu na kutatua changamoto za wateja kwa urahisi na haraka zaidi. Mpaka ifikapo mwisho wa mwaka Airtel itazindua zaidi ya maduka 2000 nchini
Mkaguzi wa Polisi wa wilaya ya Korogwe, Merkiad Makumba akikata utepe wakati wa kuzindua duka la Airtel katika wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, akishuhudia ni Afisa wa wateja wa Airtel Korogwe, Bi Elen na Meneja mauzo wa Airtel Tanga, Habibu Kiango.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...