Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali haitarudi nyuma kamwe katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini mpaka hapo vitendo hivyo vitakapokoma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa Kimataifa wa ngazi ya Juu wenye lengo la kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya Rushwa katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa vita ya kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi ni kipaumbele cha kwanza katika Serikali ya awamu ya Tano na wale wote wanaowezesha, kunufaika na kuhusika na vitendo hivyo wataendelea kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo nchini.

“Kupambana na rushwa ni jambo la msingi na muhimu kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu katika nchi yeyote Duniani,” Amesisitiza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya awamu Tano chini ya Uongozi Shupavu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inaendelea kukaza kamba katika mapambano dhidi ya rushwa ambayo kwa muda mrefu sasa yamechangia kurudisha nyuma juhudi za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Amesema Serikali ya Tanzania inalenga kufikia kipato cha kati na kuimarisha uchumi wa viwanda hadi ifikapo mwaka 2015 hivyo malengo hayo yatafanikiwa haraka iwapo tu vitendo vya rushwa vitakomeshwa katika ngazi zote nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Rais wa zamani wa nchi ya Georgia Mhe. Mikheil Saakshvili akihutubia na kutoa uzoefu wa nchi yake dhidi ya mapambano dhidi ya rushwa wakati wa ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu  Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassanakiangalia kitabu kinachoelezea mapambano dhidi ya rushwa na Rais wa zamani wa nchi ya Georgia Mhe. Mikheil Saakshvili (kushoto) wakati Ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa , Rais huyo wa zamani alitoa uzoefu wake na wa nchi yake katika kupambana na rushwa.
Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa , Rais huyo wa zamani alitoa uzoefu wake na wa nchi yake katika kupambana na rushwa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...