Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
Watendaji katika ngazi ya vijiji pamoja na kata wametakiwa kuwa na mipango madhubuti ya miradi yao kuitekeleza ili serikali iweze kuingiza katika bajeti . 
Hayo ameyasema leo Mchumi wa Halmashauri ya Mkuranga, Kaunga Amani wakati alipotembelea miradi ya ujenzi wa kituo cha afya Tengerea pamoja na Zahanati ya Dondwe. 
Kaunga amesema kuwa miradi ya ujenzi wa vituo hivyo vinatakiwa kufikia hatua ya boma ndipo Halmashauri inachukua kwa kumalizia ambavyo ni sawa na asilimia 80. 
Amesema kushiriki kwa wananchi katika miradi kutaka kuwa na umiliki wa kitu hicho kutokana na nguvu walizowekeza kaka miradi. 
Aidha amesema kuwa miradi hiyo ikifika katika hatua ya boma kati ya Agosti na Septemba mwaka huu basi wataiingiza katika bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 ili nguvu za wananchi zisipotee bure. Hata hivyo amewataka wananchi kujitoa kwa nguvu kutekeleza miradi hiyo ili kuweza kuipa kazi halmashauri katika kupanga bajeti ya miradi hiyo. 
Diwani wa Kata ya Tengerea, Shaban Manda amesema kuwa wananchi wamekuwa wakitjjitoa katika uchangiaji wa nguvu zao katika hatua za awal za miradi. Amesema kuwa katika kata hiyo hakuna zahanati wala kituo cha afya hali ambayo ni hatari kwa wananchi pamoja na wanawake wakati wa kujifungua.
Diwani wa Kata ya Tengerea, Shaban Manda akizungumza na watendaji wa Halmashauri, vijiji juu ya uharakishaji wa miradi ili serikali iweze kuipokea leo 
Mwakilishi  wa Mbunge wa Mkuranga, Omary Kisatu , Mchumi wa Halmashauri ya Mkuranga, Kaunga Amani , pamoja na  Diwani wa Kata ya Tengerea, Shaban Manda  wakitembelea  mradi wa Ujenzi wa Zahanati  katika Kijiji cha Dondwe leo.
Mchumi wa Halmashauri ya Mkuranga, Kaunga Amani akitoa maelekezo kwa watendaji Vijiji na Kata wanaotekeleza miradi ya Ujenzi wa Kituo Afya, Zahanati  leo .Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...