Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  ameonya kwamba kuanzia sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitowavumilia Madaktari wanaofanya uzembe wakati wa kutoa huduma za Afya kwa Wananchi wanafika Hospitalini kupata huduma za matibabu.
Alisema Serikali haitosita kumfukuza kazi mara moja Daktari ye yote atakayebainika kufanya uzembe  wa makusudi bila ya kujali jina au sifa alizonazo Daktari husika.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati akitoa hoja ya kuahirisha Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar lililojadili Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 2017/2018 kwenye ukumbi wa Baraza hilo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema dhamira ya Serikali kupitiA Wizara husika ya Afya ni kutoa huduma bora  yaliyobainishwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wakichangia Hotuba ya Wizara ya Afya.
Balozi alisema yapo malalamikombali mbali ya kiutendaji hasa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja yaliyojitokeza  ambayo huleta kero na maudhi kwa Wananchi wanaofika kupata huduma za matibabu.
Alitanabahisha wazi kwamba  baadhi ya Madaktari wamekuwa na tabia sugu ya kutotekeleza wajibu na majukumu yao wakati wengine wakipenda kutumia lugha chafu zinazowavunja moyo wagonjwa.
Alisema hatua hiyo inakera na kuchukiza Wananchi kutokana na kufikia huduma zinazotolewa kamwe hazilingani na fedha nyingi zinazotolewa na kugharamiwa na Serikali kwa kila Mwezi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitahadharisha kwamba vipo vifaa kufanyia uchunguzi kwa wagonjwa ambavyo kufanyiwa hujuma kwa makusudi ili wahusika wawaelekeze wagonjwa  kwenda kwenye Hospitali zao au zile wanazopewa baghshishi.
Alisema kitendo hicho kisichokubalika si cha haki kufanyiwa wagonjwa ambao wengi wao ni maskini na baadhi yao hutoka masafa ya mbali kama Vijijini kufuata huduma za matibabu Hospitali za rufaa.
Akizungumzia migogoro ya ardhi  Zanzibar licha ya Serikali kuanzisha Kamisheni ya  ardhi kwa lengo la kuodnosha migogoro hiyo kupitia Mamlaka ya Ardhi Balozi Seif alisema bado tatizo hilo halijapatiwa ufumbuzi kutokana na baadhi ya Watu hawajali kufuata sheria.
Alisema hivi sasa Kamisheni ya Ardhi ipo katika hatua za kutayarisha Sera mpya ya Ardhi, kuweka usimamizi imara wa Ardhi pamoja na upangaji wa matumizi bora ya Ardhi.
Balozi Seif alieleza kwamba Serikali kufuta maeneo yote ya Ardhi ili yarudi Serikalini na kupangwa upya.
Alifahamisha kwamba kuanzia sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitomvumilia mtu ye yote ambae atasababisha migogoro ya Ardhi hata kama ni Kiongozi au Mwananchi wa kawaida.
Baraza la Wawakilishi limeahirishwa hadi asubuhi ya Jumatano ya Tarehe 27 Septemba Mwaka huu wa 2017.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiufunga Mkutano wa Sitai wa Baraza la Tisa laWawakilishi Zanzibar uliokuwa ukijadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/2018 katika Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Chukwani nje kidogo ya Kusini mwa Mji wa Zanzibar.
 Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Baadhi ya Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotuaba ya Balozi Seif  katika Baraza la Wawakilishi Chukwani.
 Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakichukuwa dondoo kwenye  Hotuba ya kufungwa kwa  Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani.

 Wa kwanza kulia ni  Mh. Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu. Mh.Suleiman Sarahan Said Mwakilishi wa Jimbo la Chake chake na Mwakilishi wa Kuteuliwa Ikulu Mheshimiwa  Ahmeda Abdulwakil.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid akitoka  barazani baada ya kuahirishwa Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar lililojadili Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 2017/2018 kwenye ukumbi wa Baraza hilo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...