Sheikh Shariff Majini kutoka Dar es salaam Siku ya Eid Pili akiwa Arusha ameendesha Dua maalum ya kuaga Mwezi mtukufu wa Ramadhani. Sheikh aliifanya Dua hiyo katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace.
Dua ya Sheikh ilianza saa nane na kumalizika saa kumi na mbili jioni na kuhudhuriwa na wakazi wengi wa Jiji la Arusha. Pia Sheikh alipata nafasi ya kusikiliza shida mbalimbali za watu waliojitokeza katika Dua. Sheikh anataraji kuendelea na Dua Jijini Arusha siku ya Eid Tatu (Jumatano tarehe 28-06-2017) katika viwanja vya Soko la Kilombero stendi ya Hiace.
Sheikh Shariff Majini akiwasili kuendesha Dua maalum ya kuaga Mwezi mtukufu wa Ramadhani katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace jijini Arusha.
Sehemu ya umati wakati wa dua  hiyo katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace jijini Arusha.
 Sheikh Shariff Majini akiendesha Dua maalum ya kuaga Mwezi mtukufu wa Ramadhani. katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace jijini Arusha.
Sehemu ya umati wakati wa dua  hiyo katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...