Na Atley Kuni - Mwanza.

Jumla ya mizani 3,070 Iliyo Hakikiwa katika mikoa ya kanda ya ziwa kwa ajili ya matayarisho ya ununuzi wa pamba kwa msimu wa 2017/2018 imekutwa salama baada ya kuhakikiwa na wakala wa Vipimo nchini.

Akizungumza nami Jijini Mwanza, kaimu Meneja Sehemu ya Elimu, Habari na Mawasiliano Bi. Irene John, amesema, Wakala wa vipimo Tanzania ( WMA) chini ya usimamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeendelea kutoa elimu kwa wakulima pamoja na kuhakiki mizani itakayotumika kununulia zao la Pamba ikiwa ni maandalizi ya msimu wa ununuzi wa Pamba kwa mwaka huu.
Wakulima mkoani Shinyanga wakipatiwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Mizani kabla ya msimu kuanza. 

Bi. Irene amesema, Dhumuni kuu la utoaji elimu kwa wakulima wa zao la Pamba Kanda ya Ziwa ni kuwawezesha wakulima kutambua mizani iliyosahihi (inayoruhusiwa kwa biashara) na ile iliyochezewa (isiyoruhusiwa kwa biashara) ili waweze kujilinda wenyewe pindi maafisa vipimo wanapokuwa hawapo katika vituo vya kuuzia Pamba yao, lakini pia ni kuwawezesha wakulima kupata faida ya thamani kamili ya jasho lao.

Ameongeza kuwa, katika maandalizi ya msimu mpya wa ununuzi wa Pamba zaidi ya mizani 1,402 imekaguliwa katika mkoa wa Shinyanga, mkoa wa Simiyu wamekagua zaidi ya mizani 302, mkoa wa Geita jumla ya mizani 40 tayari imekaguliwa, ilihali katika mkoa wa Mwanza wamekagua mizani 448, mkoa wa Mara mizani 690, mkoa wa Tabora wamekagua mizani 164 pamoja na mkoa wa Kagera wamekagua jumla ya mizani 24 ikiwa ni maandalizi ya ununuzi wa zao la Pamba.
Wakulima mkoani Geita wakipatiwa Elimu. 

Katika hatua nyingine Irene amesema, sheria ya Vipimo Sura 340 inawataka Wakala wa Vipimo kuhakiki na kupiga chapa vipimo vyote vinavyotumika katika biashara ikiwa ni pamoja na kuweka sticker kwa kipimo kitakachokuwa tayari kimehakikiwa na kukutwa kikiwa sahihi ili iwe rahisi kwa wakulima kuona na kutambua mizani iliyokaguliwa na kuruhusiwa kwa biashara kwa mwaka husika.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...