Na Judith Ferdinand wa BMG, Mwanza
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoani Mwanza Mhe. Susan  Maselle, ametoa shilingi milioni moja ili kuchangia ujenzi wa darasa la awali (chekechea) katika shule ya msingi Nyerere, Kata ya Igoma Jijini Mwanza.
Mhe. Maselle alitoa fedha hizo jana katika harambee ya kuchangia ujenzi huo, iliyofanyika katika ukumbi wa Agape Lodge katika mtaa wa Nyerere Kata ya Igoma.
Alisema pamoja na juhudi za serikali kuboresha elimu, bado sekta hiyo haijafika pale panapohitajika ambapo alitoa wito kwa wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wabunge kuona umuhimu wa kuchangia masuala ya kuboresha elimu kwa kujitoa na kuchangia kama alivyofanya yeye. 
 Aidha aliwaomba wazazi wenye uwezo kuchangia elimu ili kupata viongozi wa baadae na kuwajenga katika kusaidia na kujitoa katika jamii.
Katibu wa Baraza la Vijana Chadema BAVICHA mkoa wa Mwanza, Boniphace Nkobe, aliwasihi wadau wote kuungana kwa pamoja ili kukamilisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati ili wanafunzi waweze kusoma wakiwa darasani kama wanafunzi wengine.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Igoma Mashariki, Odoyo Lan’go alisema sera ya serikali katika elimu inamtaka mtoto kabla hajaanza darasa la kwanza (elimu ya msingi) awe amepitia elimu ya awali, hivyo wadau wanatakiwa kuchangia kukamilika kwa darasa hilo la awali

Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mkoa Wa Mwanza Mhe.  Susan Maselle, akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa darasa la awali katika shule ya Msingi Nyerere Jijini Mwanza..

Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mkoa Wa Mwanza, Susan  Maselle akiwa na wazazi, watoto na viongozi wa Mtaa wa Nyerere Jijini Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...