MFANYAKAZI wa Tanesco mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga, ameibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko katika droo ya 25 iliyochezeshwa jana, jijini Dar es Salaam. 

Lukinga fundi wa Tanesco alitangazwa mshindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

Akizungumza katika droo hiyo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema ni mara ya kwanza kumpata mshindi wa droo kubwa ya Sh Milioni kutoka Mkoa wa Mtwara.

Alisema kupatikana kwa mshindi huyo kunaongeza wigo wa washindi wa Biko kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wanaoshinda droo kubwa pamoja na wanaoibuka na zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja. 

“Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mchezo wetu wa kubahatisha tumempata mshindi kutoka Mtwara, ambaye ni fundi wa Tanesco, huku tukiamini kuwa kila mtu anaweza kuibuka na ushindi kutoka Biko endapo atacheza mara nyingi zaidi kwa kupitia mitandao ya simu.

“Biko inachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba yetu ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456, huku gharama za uchezaji zikianzia Sh 1,000 na kuendelea, ambapo shilingi 1000 inatoa nafasi mbili ambazo ni ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya Sh Milioni 20 inayotolewa kila Jumatano na Jumapili,” Alisema Melles. 
 
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed kushoto akiandika maelezo ya mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20 alilopata mfanyakazi wa TANESCO Mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga mara baada ya kupatikana kwenye droo ya 25 iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...