Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Yanga, Dismas Ten
Na Agness Francis, Globu ya Jamii.
Winga machachari wa timu ya Yanga Simon Msuva anatarajiwa kuondoka kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya vipimo ili kujiunga na timu ya ya Difaa Hassani Eljadidi (DHJFC) inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Yanga, Dismas Ten amesema kuwa mchezaji Saimon Msuva anatarajia kuondoka kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya zoezi la vipimo vya afya ili kukamilisha mchakato katika timu ya Difaa Hassani Eljadidi (DHJFC).
Ten amesema walishamaliza mazungumzo na klabu hiyo kwa ajili ya kujiunga nao na wamempa baraka zote kijana wao kwa ajili ya kuanza maisha mapya ya soka nchini Morocco.
Timu hiyo ambayo msimu uliopita ilishikilia nafasi ya pili katika nmsimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 59, huku WCA Casablanca wakiwa kilelelni kwa point 66 katika ligi kuu ya Morocco inayojumuisha timu 16 kama ilivyo ligi kuu ya Tanzania bara.
Hata hivyo uongozi wa Yanga unasubiri majibu ya vipimo vya Msuva na kuendelea na taratibu zote za kuuzwa kwa mchezaji huyo ambaye ameitumikia club hiyo misimu 5 akiwa kiungo mshambuliaji mwenye jezi namba 27.
Jana mchana Msuva alikwenda klabu ya Yanga kuaga na kupata baraka za viongozi wake waliokuwa nae katika maisha ya soka ndani ya Klabu ya Yanga kwa miaka mitano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...