Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania, Ibrahim Mussa (kushoto) alipokuwa akimueleza mambo mbalimbali ya uhifadhi na changomoto zake inapokuja suala la kushirikisha vyombo vya habari kabla ya kufungua mkutano wa sita wa wahariri na wanahabari waandamizi unaohusu sekta ya utalii nchini ambao umeandaliwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA) unaofanyika jijini Tanga 27 - 29, Julai 2017. Pichani kati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Allan Kijazi 
 
Katika mkutano huo Prof  Silayo atawasilisha mada "uhifadhi wa misitu ya hifadhi ya asili na mpango mkakati wa utalii Kesho Ijumaa ya tarehe 28 Julai 2017 saa 05:45 asubuhi na kurushwa moja kwa moja kupitia ukurasa wa facebook wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (www.facebook.com/foresttz). 
 

usikose kuungana naye na atajibu maswali yatakayoibuka kutokana na mada atakayoiwakilisha!

Mratibu wa Mradi wa Misitu ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Tanzania, Gerald Kamwenda (Kushoto) akijadiliana jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof Dos Santos Silayo mara baada ya kupokea taarifa za wajumbe wa Mkuno Mkuu wa Mwaka wa Wahariri na Wanahabari Waandamizi ulioandaliwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kutembelea Hifadhi ya Misitu Asilia ya Amani Siku ya Jumamosi (Julai 29,2017).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...