Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi, CUF linaloongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba limewavua uanachama wabunge nane wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu, yakiwemo kukisaliti chama hicho.
Mwenyekiti huyo wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, amesema, baraza pia limewavua uanachama madiwani wawili wa viti maalumu mkoani Dar es Salaam kwa makosa kama hayo.
 Profesa Lipumba ametangaza uamuzi huo leo wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika makao makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam. Amesema wabunge hao nane ni kati ya 10 walioitwa hivi karibuni na Kamati ya Maadili na Nidhamu kwa mahojiano wakitakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili za kukihujumu chama hicho kwa maelezo kuwa walitaka kushirikiana na CHADEMA kumwondoa yeye madarakani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...