Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh.  Aggrey Mwanri amezindua rasmi kambi maalum ya huduma za Afya juu ya upimaji wa Afya bure kwa wananchi mbalimbali Wilayani Nzega, ndani ya Hospitali ya Wilaya ya Nzega. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanri ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliwapongeza waandaaji wa kambi hiyo kwani itasaidia kuboresha afya za wananchi ili kuwa na afya njema.

“Wananchi wanahitaji Afya njema, tunapongeza kwa kambi hii kwani madaktari bingwa waliokuja hapa watatua matatizo ya msingi kwenye afya zetu. Hivyo wananchi mujitokeze kwa wingi” aleleza RC Mwanri. Aidha, Mh. Mwanri amewapongeza  Madaktari bingwa kutoka China ambao wanaendesha kambi hiyo ya siku Sita, iliyoanza rasmi Julai 24 na inatarajia kumalizika Julai 30.
Hata hivyo, Mh. Mwanri aliwaagiza Wakurugenzi wote wa Mkoa wa Tabora waupokee mpango huo wa kambi za huduma za Afya ili uende mkoa mzima kwani wanakosa fursa ya kuonana na Madaktari bingwa.

“Ni jambo zuri, tunaomba Wakurugenzi wote mulipokee suala ili wa Mkoa wa Tabora ili liendelee Mkoa mzima. Pia ni wasaha kwa wananchi wote kupeana taarifa ili zienee kwa watu wote wajitokeze hapa Nzega kupatiwa huduma za upimaji na matibabu.” 
Alieleza Mh. Mwanri huku akimuagiza Mganga Mkuu ahakikishe anaratibu mpango huo uenee Mkoa nzima wa Tabora.

Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini ameshukuru Serikali ya China kwa kufanikisha tukio hilo ikiwemo kutoa dawa za Maralia kwani kwa msingi huo utasaidia kuokoa maisha ya wananchi wa Nzega.
“Tunapokea kwa mikono miwili msaada huu wa kutoka Serikali ya China hasa kupitia kwa Balozi wake hapa nchini Tanzania. Dawa hizi ni nyingi nahakika zitasaidia wananchi wote kuanzia wilaya ya Nzega na Mkoa nzima wa Tabora kwa ujumla. Nawashukuru sana wananchi wanaojitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuja kupata  huduma za matibabu kwenye kambi hii ya madaktari bingwa hapa Nzega” alieleza Dak. Kigwangalla.

Zoezi hilo la Upimajj wa Afya Bure Wilayani Nzega, limeandaliwa na Wabunge wa majimbo yote ya  Nzega ambapo imeanza kuanzia hiyo Julai 24 na itatarajiakumalizika Julai 30, huku kwa wakazi wote wa Nzega na jirani wata pima afya zao bure na kupata huduma za matibabu bure, ikiwemo upasuaji. Tayari timu ya Madaktari bingwa wa kila fani ya tiba wapo kwenye kambi hiyo inayoendelea kwenye Hospitali ya Wilaya ya Nzega.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...