Na Pamela Mollel,Arusha

Serikali imewataka viongozi wa chama cha wafugaji Tanzania pamoja na watetezi wa haki za wafugaji kuhakikisha wanaondoa migogoro ya wafugaji na wakulima, ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara Nchini hali ambayo imekuwa ikirUdisha maendeleo nyuma

Akizungumza jijini hapa katika ufunguzi wa warsha ya siku tatu iliyowakutanisha watetezi wa haki za wafugaji nchini ,Katibu Tawala Wilaya ya Arusha David Mwakiposa alisema kuwa lengo la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo hao watetezi ili waweze kuondoa migogoro inayojitokeza katika jamii

“Serikali tunaomba sana watetetezi wa haki za wafugaji kuangalia kwa uzito wa kipekee kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima na wahamasishe uwanzishwaji wa viwanda vya kuchakata bidhaa za mifugo ili kumuunga mkono Raisi Magufuli katika sera ya viwanda”Alisema Mwakiposa

Aidha alisema kuwa sekta ya wafugaji na kilimo inaajiri watanzania walio wengi zaidia asilimia 70 na ndio sekta pekee ambayo haiitaji elimu kubwa tofauti na ajira za viwandani na sehemu nyingine hivyo ni muhimu kujengwa uwezo ili kutimiza sera ya viwanda hapa nchini

Katibu Tawala Wilaya ya Arusha David Mwakiposa akizungumza leo katika warsha ya siku tatu jijini Arusha iliyowakutanisha watetezi wa haki za wafugaji nchini , mafunzo hayo yanalengo la kuwajengea uwezo watetezi hao ili waweze kuondoa migogoro inayojitokeza katika jamii(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha).Washiriki wa semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Arusha kwa semina ya siku tatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...