Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Timu ya riadha ya vijana chini ya miaka 17 imeleta
heshima kubwa kwa nchi yetu baada ya kurejea na medali ya shaba aliyoshinda
kijana Francis Damasi katika mbio za
mita 3000 kwenye mashindano ya Jumiya ya
Madola yaliyomalizika hivi karibuni huko
nchini India.
Medali ya shaba katika mahindano ya riadha iliyoletwa na kijana Francis imerejea tena
baada ya miaka 19 tangu Tanzania ilivoshinda medali hiyo mwaka 2008 katika michezo
hiyo.
Timu hiyo iliyorejea nchini leo imepokelewa na
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo
ameeleza kufurahishwa na matokeo hayo mazuri waliyopata wanariadha hao
ambao wameitangaza vyema Tanzania.
“Vijana mmefanya vizuri sana katika mashindano
haya Serikali tunawapongeza sana kwa
kuitangaza nchi yetu lakini pia kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu katika
mashindano haya nawaahidi kuendelea kushirikiana na uongozi na wadau wa riadha
nchini ili tufike mbali zaidi” Alisema Prof. Elisante Ole Gabriel.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa chama cha riadha
nchini Bw. Filbert Bayi amesema kuwa
mchezo wa riadha kwa sasa ni mchezo ambao umeitangaza Tanzania kwa kiasi
kikubwa kutokana na kushiriki mashindano
mengi ya Kimataifa hivyo ni vyema wadau wakajitokeza kwa wingi kuwekeza katika
mchezo huo ambao umeendelea kuletea heshima Taifa.
“Riadha imeitangaza Tanzania na itaendelea
kuitangaza hivyo wadau wanapaswa kuona fursa hii na kuwekeza katika mchezo huu
ili ufike mbali,kila mtu katika eneo lake aone fursa hii na aitumie kwa manufaa
ya kizazi hiki na kitakachokuja” Alisema Bw. Bayi.
Naye Kijana Francis Damian aliyepata medali hiyo
baada kushinda mbio za mita 3000 ameeleza kufurahishwa na ushindi huo kwani
alijiandaa na alizingatia maelekezo ya walimu wake yaliyompelekea kupata
ushindi huo na ameshauri vijana kama yeye kuthubutu na kuamini kuwa wanaweza
kwani mchezo huo ni mzuri na una mafanikio makubwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akimpongeza mwanariadha Francis
Damas leo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa kupata ushindi
wa medali ya shaba baada ya kushinda mbio za mita 3000 katika mashindano ya
Jumuiya ya madola chini ya miaka 17 yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini Bahamas
Katibu Mkuu chama cha Riadha nchini Bw. Filbert
Bayi (aliyesimama) akizungumza na
wanariadha na wadau wa mchezo huo mara baada ya timu ya riadha ya vijana chini
ya miaka 17 kurejea nchini na medali ya shaba katika mashindano ya Jumuiya ya
Madola yaliyoalizika hivi karibuni huko Bahamas.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea Bendera ya Tanzania kutoka kwa mwanariadha
Regina Mpigachai mara baada ya kurejea nchini na ushindi wa medali ya
shaba katika mashindano ya Jumuiya ya madola chini ya miaka 17 yaliyomalizika
hivi karibuni huko nchini Bahamas.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi msaidizi wa
maendeleo ya michezo wa Wizara hiyo Bw. Alex Nkenyenge.
Mkuu wa Msafara na mwalimu wa wanariadha Bibi
Mwinga Mwanjala akitoa neno la shukrani
mara baada ya kurejea nchini na
ushindi wa medali ya shaba katika mashindano ya Jumuiya ya madola chini
ya miaka 17 yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini Bahamas.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...