Ujumbe kutoka Ubalozi wa Israel nchini Kenya umetembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo. Maestro Nir Brand akipiga kinanda ili kuwaburudisha watoto wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Ofisa Uhusiano kutoka ubalozi huo, Angela Mogusu.  
 Watoto wanaotibiwa katika hospitali hiyo wakisikiliza moja wa wimbo uliokuwa ikiimbwa na Brand leo kwenye Jengo la watoto.
 Watoto wakicheza na Daktari Bingwa wa Watoto, Rehema Laiti leo.
  Ilala Brand akipiga makofi ikiwa ni sehemu ya kuungana wagonjwa leo.



 Dk. Shlomi Cohen akishiriki katika shughuli ya kuimba na kucheza na watoto hao leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ankal,

    Za masiku? Nimevutiwa na hii taarifa. Nimejifunza na kujione huku ughaibuni kuwa siku hizi wanatambua na kutumia sanaa kwa namna mbali mbali ikiwmo katika matibabu. Kuna dhana kama "art therapy" na hii inayoelezwa katika taarifa yako huitwa "music therapy." Hii "art therapy" inajumlisha pia burudani ya hadithi.

    Katika kutafakari suala hili, nimetambua kuwa wale waganga wetu wa enzi za wahenga walikuwa wanafanya sawa walipokuwa wanaimba, au wanapiga ngoma na ala zingine za muziki katika aina fulani fulani za matibabu. Wazungu walikosea walipopuuza jadi zetu hizi na kuziita za kishenzi. Ila sasa, kama nilivyotamka hapa juu, nao wameamka usingizini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...